Friday, September 26, 2014
Thursday, September 25, 2014
WADAU WASAIDIE WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI (ALBINO) KUPATA MATIBABU YA SARATANI YA NGOZI
WATU wenye ulemavu wa ngozi (albino), wamekuwa
wakisumbuliwa na maradhi ya ngozi hususan saratani ya ngozi.
Maradhi hayo hadi sasa, baadhi ya watu huyachukulia kuwa
labda hayana tiba, hiyo inatokana na jamii kuwatelekeza wapatwapo na maradhi
hayo. Jamii inapaswa kutambua kuwa maradhi hayo yana tiba
kinyume inavyodhaniwa na baadhi ya watu. Kutokana na mazingira hayo, serikali kupitia Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii imeweka mazingira mazuri ya kuwapatia matibabu watu hao
wenye wenye ulemavu wa ngozi. Mazingira hayo yatawasaidia albino kujikinga na ugonjwa
huo wa saratani ya ngozi, kulinda afya zao.
Rai kama hiyo imekuwa ikitolewa mara kadhaa na baadhi ya
wataalamu wa magonjwa hao. Miongoni mwa wataalamu hao baadhi yao ni madaktari
Bingwa wa magonjwa ya ngozi na afya ya jamii kutoka Hosipitali ya Rufaa ya
KCMC. Kauli kama hiyo waliwahi kuitoa wakati akitoa huduma kwa
walemavu wa ngozi katika Hospitali ya Mkoa wa Mwanza ya Sekou Toure kupitia
ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la Standing Voice.
Ushari huo unapaswa kufanyiwa kazi kwa sababu idadi ya
watu wenye ulemavu wa ngozi nchini ni kubwa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. Ieleweke kuwa maradhi ya saratani ya ngozi ni tatizo kwa
taifa hata hivyo, waathirika wakitibiwa mapema wanaweza kuepuka kupata kansa
hiyo.
Aidha, ni wakati kwa wadau na taasisi mbalimbali kuungana
kuwasaidia kimatibabu albino ambao
wanaonekana kupatwa na maradhi hayo. Kwa mfano kulikuwa na Shirika lisilokuwa la kiserikali
lenye makao yake makuu nchini Uingereza (Standing Voice ni), limewahi kufadhili huduma hiyo. Kipindi hicho shirika hilo liliamua kuwafadhili albino
waliokuwa wakishindwa kusafiri kufuata huduma hiyo katika Hospitali ya KCMC au
Ocean Road.
Tukubali kuwa tatizo hilo bado lipo na linazidi kukuwa
katika maeneo mbalimbali nchini, hivyo basi kila Mtanzania atumie nafasi yake
kuwasaidia watu hao wenye ulemavu wa ngozi.
Chanzo: Tanzania Daima
Tuesday, September 23, 2014
Tumikia kwa Huruma (Serve with Compassion)
Ilikuwa ni shughuli ya kusafisha masikio, kutibu matatizo
madogo madogo ya masikio na kwa wale ambao ni viziwi walikuwa wakipimwa na
kisha kutengenezewa "shimesikio" earmould yaani umbile la sikio kwa
ajili ya kutengenezewa hearing aid. kazi hii ilikuwa inaendeshwa na wadhamin
toka Marekani "STARKEY HEARING FOUNDATION" Manesi na Madaktari toka
Sekoture pamoja na Walimu wanaofundisha watoto viziwi. Ilikuwa ni kwa watu wote
wenye shida ya masikio pamoja na viziwi wa hapa Mwanza. Tulianza siku ya ijumaa
tarehe 19/09 na kumalizika jumapili hii ya tarehe 21/09 hapa Nyanza S/M.
![]() |
| Mwl Fubusa (katikati) akiwa na wenzake tayari kwa kuanza upimaji wa masikio |
![]() |
| Mwl Fubusa akipima sikio la mwanafunzi |
Monday, September 22, 2014
Nani Ataomba Msamaha kwa Unyama wanaotendewa watu wenye Ulemavu?
Ni kawaida ya binadamu atambuapo kuwa alifanya kosa lenye kugharimu nafsi za watu kwa namna moja au nyingine huomba msamaha. Uingereza waliomba msamaha kwa kuanzisha biashara ya utumwa; Papa kwa niaba ya Warumi aliomba msamaha kwa unyama waliomfanyia Bwana Yesu; Ujerumani waliomba msamaha kwa unyama waliowafanyia Wayahudi kwa kuwaua takribani milioni sita Wayahudi hao.
Je, kwa unyama ambao watu wenye ulemavu waliwekwa kwenye chemba ya gesi wakati wa utawala wa Hitler nani ataomba msamaha?
Je, unyama uliofanywa kwa watu wenye ulemavu kwenye "Eugenics Movements-the war against the weak" nani ataomba msamaha?
Je, ni nani mwenye ujasiri atakaye kuja mbele za watu na kuomba msamaha kwa mauaji ya albino nchini Tanzania?
Je, ni nani atakayethubutu kuomba msamaha kwa tamaduni kandamizi kwa watu wenye ulemavu?
| Cheti cha uthibitisho kuwa mtu hana ulemavu. Watu wote waliokutwa na ulemavu waliuawa |
Tafadhali! Piga hatua moja tu ya kufikiri juu ya hili!
Sunday, September 21, 2014
If you Don't help them; Don't hurt them
Every person needs to be respected and be regarded in every aspect of life. If you don't help other people for any reason, it is well with your soul, but don't hurt them.
This is relevant to the famous quote of Dalai Lama that;
"Our prime purpose in
this life is to help others. And if you can't help them, at least don't hurt
them."
Think about it!
Saturday, September 20, 2014
Ajali za barabarani zinaongeza idadi ya watu wenye ulemavu
Mojawapo ya vyanzo vya mtu kuupata ulemavu ni pamoja na ajali anuai kwenye mazingira yetu. Mifano ya ajali ni pamoja na zile za magari, pikipiki, kwenye michezo nk.
Nimeshuhudia marafiki wengi ambao maisha yao yalikuwa mazuri na yenye kuvuta furaha, waliishi kwa kudhani ulemavu ni kwa jirani yake tu; lakini mara baada ya kupata ulemavu wamepotea kabisa kwenye ramani ya jamii. Waliokuwa wanasiasa imara hawavumi tena, waliokuwa na uchumi mzuri wameyumba, waliokuwa wanajihisi wanathamani kuliko watu wenye ulemavu kwa sasa wanajiona si binadamu. Hizi zote ni athari za kuwa na mtazamo hasi juu ya ulemavu na watu wenye ulemavu.
Hakika Mungu aturehemu na kutuhurumia!
Subscribe to:
Posts (Atom)



