Saturday, February 7, 2015
Thursday, January 8, 2015
Disability awareness, feeling it!

In the past years, especially in African continent, particularly in Tanzania- my motherland; disability matters and people with disabilities were not openly discussed. The issue was treated secretly by the chosen elders! Of course, it was considered a taboo.
Nowadays things are different. People, with and without disabilities can articulate any utterance to suit people with disabilities. Indeed, it is a high time to talk more and more about disability affairs due to several facts. Presently, the two scenes are the key issues to be discussed; one: to educate people about disability and people with disabilities of their crucial human rights and; secondly- drawing the attention to the mass about effects of present poisonous world chemicals, and that, every person is now becoming a prime suspect for being attacked by disability content.
1. We are required to wear and hold strong sense about disability...
2. We need to educate others and be educated of disability concepts...
3. We need to, for us, people with disabilities and the families caring for people with disabilities, tell others what real disability is, putting into the practical ways about the long and immediate effects inherent with it...
See what Oscar Pistorius said...
"I have a strong sense that I have to educate people about disability."
He further said...
"My parents didn't give me any scope to feel sorry for myself. They were just like 'go play with your brother, go climb a tree, go fall off your motorbike, do whatever you want. Don't come crying to us when you get scratched. You've got prosthetic legs - that's very nice.''
Talk openly, discuss freely, feel lucky, and assume privileged to argue about disability and people with disabilities...the central theme being "creating a powerful world to suit every individual in it."
Wednesday, January 7, 2015
Maoni ya watu kuhusu mauaji ya Albino Tanzania
Baby Madaha
Ni kwa sababu wananchi hawatoi ushirikiano unaotakiwa kwa wana-usalama, jambo linalosababisha kazi ya kuwabaini wauaji kuwa ngumu.
|
Coletha
Serikali haiwezi kushindwa kwa sababu wao ndiyo wenye kila kitu, polisi, jeshi usalama wa taifa na mahakama ni yao, sasa hapo wanashindwaje? Kama siyo udhaifu, tena wa makusudi dhidi ya wananchi katika utendaji kazi, wao ndiyo wenye wajibu wa kuwalinda wananchi wao.
|
Bi Mwenda
Wanawaonea sana, kwa kweli tangu wameanza kuwaua hakuna mabadiliko yoyote ya kimaendeleo waliyopata, pengine hata hao wanaopaswa kuzuia nao ni wahusika ndiyo maana kuna ugumu.
|
William Mtitu.
Mimi napendekeza atakayemkata mkono mmoja albino akishikwa akatwe mikono 2 na mguu mmoja ili iwe fundisho.Lakini pia itolewe elimu ya kutosha kuwa huwezi kutajirika kwa kiungo cha albino, kama kuna mtu anaamini anaweza basi aliyekamatwa na kiungo apelekwe baharini au ziwani avue samaki aone kama atavua samaki wengi, mahakama zitoe hukumu mapema zinapochelewesha maamuzi, ukatili na mauaji unaendelea.
|
Hussein Machozi
Serikali yenyewe ndiyo inawapa nguvu wauaji, na sisi inatufumba macho tu kuwa inawafuatilia. Rushwa kwa vyombo vinavyohusika na mauaji ya albino pia ni tatizo, serikali yenye nguvu ndiyo sababu ya hao wenzetu kufa mimi na wewe hatuna nguvu ya kuzuia hata robo.
|
Tuesday, January 6, 2015
Jifunze chanzo cha ualbino

By Neristera Kihoza
Albino ni watu wenye
ulemavu wa ngozi unaosababishwa na ukosefu wa madini aina ya melanin mwilini
ambapo madini haya husababisha kutokuwepo kwa rangi nyeusi kwenye ngozi na
nywele pia, hivo basi wanandoa wanapokutana kimwili kwa lengo la kutafuta
mtoto, kama mmoja wao ana madini haya, haijalishi ni albino au sio, kuna
uwezekano mkubwa wa kujifungua mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (albino).
Kwa hiyo mtu yeyote
akijifungua mtoto mwenye ulemavu wa ngozi sio laana, mikosi, wala balaa n.k kwa mtu huyo kama jamii kubwa ya kitanzania
inavyoamini. Naomba tufunguke sasa ili tuwaone kuwa nao ni watu wa kawaida kama
wewe na mimi, tofauti tu ni ngozi ila shughuli zote anaweza kuzifanya.
Nanyi washirikina mnaotaka utajiri wa haraka haraka kwa kutumia viungo
vya binadamu wenzenu hivi hiyo dhambi mtaitubu wapi? Mmewafanya wenzetu kuwa
wakimbizi kwenye nchi yao wenyewe kweli! na hata kutengana na familia zao! Naomba
tutoke mapangoni jamani! Kwanini wenzetu wa nchi za nje hawana haya mauzauza?
Leo hii nimepata taarifa kuwa kuna mtoto mwenye ulemavu wa ngozi aitwaye
Upendo Emanuel wa Mkoa wa Mwanza wilaya ya Kwimba ametoroshwa na wajinga
wachache wasiowatakia heri wenzetu, cha ajabu sasa eti hata watu wanaojiita eti
ni wasomi bado wana dhana potofu dhidi ya albino.
Naomba wewe mwenye upendo na hawa wenzetu tuungane pamoja ili
tuwaelimishe watu waweze kuondokana na ubaya huu pengine shetani amewakamata
pasipo kujitambua. Mwisho nawaomba watanzania wote tujenge hali ya upendo kwa
watu wenye ulemavu wa ngozi tule nao, tucheze nao na hata kushirikiana kwa
mambo yote, kwani wengine huogopa hata kuwagusa jamani! Tusiwatenge kwa sababu
we are under the same sun, mimi nawapenda sana hawa ndugu zangu.
Ubarikiwe sana kwa ushirikiano wako!
Nelistera Kihoza aonya juu ya dhana potofu ya ulemavu

Huyu ni mwalimu wa Elimu Maalum Kanda ya Ziwa. Anajua ugumu wa kumwelimisha mtu kuhusu dhana ya ulemavu. Anachotamani ni watu wote kuona umuhimu wa haki za binadamu kuzingatiwa ili kutoa fursa sawa kwa binadamu wote.
Haya ndiyo maneno yake:
"Ewe Mtanzania, uwe Mkristo, Muislam au Mpagani; unapaswa kutambua kwamba walemavu wa aina zote nao wanathamani kubwa mbinguni na duniani kama wewe ulivyo. Shida tu ni ule mtazamo potofu juu ya watu hawa; lakini wanao uwezo wa kufanya kila kitu unachoweza kufanya wewe, Ewe mzazi mpeleke shule mtoto wako ambaye ni mlemavu, kwani naye anayo haki ya kusoma kama watoto wengine. Achana na mtazamo potofu hiyo ambayo haijengi bali inabomoa. Napenda kuishauri serikali nayo pia isiwe na
mtazamo potofu juu ya watu wenye ulemavu
kwamba wanaweza kuajiriwa ktk sekta baadhi na sekta na sekta zingine hawawezi,
sio hivo, Nao wapewe fursa mbalimbali ilimradi tu wana sifa za kitaaluma
husika, Lakini pia walimu wanaofundisha wanafunzi wenye ulemavu wana kazi kubwa
sana kuliko tunavyofikiria, hivyo nashauri wapewe motisha ya kutosha
Mwisho Biblia
inasema 'huyu na wazazi wake wote hawana dhambi bali kazi ya Mungu idhihirishwe
ndani yake'. Kwa hiyo tusiwanyanyase."
![]() |
| Wanafunzi wa shule ya msingi ya wasioona Furaha, Tabora. |
Mkuu wa mkoa Mwanza atoa siku tano kwa wanakijiji kwimba kuhakikisha wanampata mtoto mwenye ulemavu wa ngozi.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo ametoa muda wa siku
tano kwa wakazi wa kijiji cha Ndami na jeshi la jadi Sungusungu wilayani
kwimba, kuhakikisha wanampata mtoto mwenye ulemavu wa ngozi – Alibinism, Pendo
Emanuel akiwa hai au amekufa ikiwa ni pamoja na wahusika wa tukio hilo
kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya dola.
Agizo hili la mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo,
linakuja kufuatia watu wasiojulikana kumuiba mtoto Pendo Emanuel mwenye ulemavu
wa ngozi majira ya saa 4 usiku Desemba 27 mwaka jana nyumbani kwao katika
kijiji cha Ndami na kutoweka naye kusikojulikana, mkasa ambao umeilazimu kamati
ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mwanza kuapa kuwa serikali haitalala usingizi
mpaka mtoto huyo mwenye umri wa miaka minne apatikane.
Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi mkoa wa
Mwanza Alfred Kapole amesema kuwa miongoni mwa kesi 72 zilizokuwa mahakamani
zikihusu mauaji ya walemavu wa ngozi, ni kesi tatu ndizo zilizotolewa hukumu
mpaka sasa, huku akiilaumu ofisi ya mkemia mkuu wa serikali pamoja na mahakama
kwa kuchelewesha kesi hizo.
Mama mzazi wa mtoto Pendo, Bi. Sophia Juma pamoja na
mkurugenzi wa shirika lisilokuwa la kiserikali la Chiriko Bi. Specioza Kasoli
wamesema kila mtu ana haki ya kuishi na kulindwa na kuongeza kwamba mtoto huyo
ni kati ya watu 74 wenye ulemavu wa ngozi wilayani kwimba na alikuwa ni mtu wa
9 kwa kupatiwa ulinzi.
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza Valentino Mlowola amesema
tayari askari polisi wamepiga kambi katika kijiji hicho kwa kazi moja tu ya
kuhakikisha mtoto huyo anapatikana, lakini pia watuhumiwa wanasakwa kwa udi na
uvumba ili wafikishwe mahakamani kwa kosa la jinai.
Chanzo: ITV Tanzania
Monday, January 5, 2015
How do we protect our albinos in Tanzania?
Police in Tanzania have arrested four people over the kidnapping of an albino girl in the north of the country, where many are killed and their body parts sold as lucky charms.
Four-year-old Pendo Emmanuelle Nundi was snatched on Saturday from her home in the Mwanza region by attackers armed with machetes, regional police chief Valentino Mlowola said.
"We have arrested four people, including the girl's father," Mr Mlowola said.
"We are still in the process of interrogating them so we can find out where the girl is - if she is still alive," the official said.
At least 74 albinos have been murdered in the east African country since 2000, according to United Nations experts.
After a spike in killings in 2009, the government placed youngsters in children's homes in a desperate effort to defend them.
A hereditary genetic condition which causes a total absence of pigmentation in the skin, hair and eyes, albinism affects one in 1,400 Tanzanians, often as a result of inbreeding, experts say.
In the West, it affects just one person in 20,000.
In August 2014, a UN rights expert warned that attacks against albinos were on the rise because Tanzania's October 2015 presidential election was on the horizon, encouraging political campaigners to turn to influential sorcerers for support.
Albino body parts sell for about $US600 in Tanzania, with an entire body fetching $75,000.
Subscribe to:
Posts (Atom)


