Monday, September 9, 2013

Ifahamu "Buddy Bike"

TEKNOLOJIA JUMUISHI

Hii ni dhana inayojaribu kusisitiza kuwa kunapotokea utengenezaji wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya binadamu kwenye jamii yoyote lazima kuwepo na usawa. Hii inamaanisha kuwa watu wenye ulemavu nao wanaweza wakatafutiwa mbinu mbadala ili wasiachwe nyuma na maendeleo ya teknolojia katika maisha.

Leo tuangalie aina hii maarufu ya baiskeli jumuishi iitwayo "BUDDY BIKE".

"BUDDY BIKE" ni aina ya baiskeli yenye viti viwili, staring mbili, pedel mbili na huendeshwa na watu wawili.

Huwa wanapanda watu wawili, mmoja anayeona na mwingine asiyeona (blind). Kazi ya asiyeona ni kupiga pedel na kazi ya anayeona ni kuongoza njia. Aina hii ya baiskeli hutengenezwa nchi za ulaya na zimesambazwa katika nchi nyingi zinazoendelea ikiwemo Tanzania (point of reference being Buigiri School For the Blind in Dodoma). Bahati mbaya baiskeli hizi zikiharibika ni vigumu kupata spea zake.

Ni aina ya baiskeli ambayo waumini wa jamii jumuishi wanaamini inaweza kurejesha heshima na ubinadamu kwa watu wasioona (blind people).

Angalia picha mbalimali za baiskeli hii hapa chini...



















Fikiri Kijumuishi ~~~ Tenda Kijumuishi ~~~ Jenga Taifa Jumuishi.