Polisi nchini China
wamemkamata mtu asiyekuwa na mikono akiendesha gari. Bwana huyo Wo Guo (45) si
tu kwamba hakuwa na leseni bali alikuwa akitumia mguu wake wa kulia kubadili
gia huku mguu wa kushoto ukikanyaga mafuta na breki.
Msemaji wa polisi amesema:
"Ni jambo la ajabu, lakini ni hatari sana kwake kuendesha gari."
Polisi huyo amesema itakuwa vyema kama ataajiri dereva wa kumuendesha. Gari la
bwana Wo linashikiliwa na polisi ili kumzuia asiendelee kuendesha.
Bwana WO akiendesha gari |
Bwana WO akihojiwa na askari polisi |
Picha na taarifa kutoka
Metro na CEN.