Monday, February 23, 2015

Maandamano ya kupinga mauaji ya albino nchini Tanzania ni machi 15, 2015




By @mdimuz IMETOSHA CAMPAIGN UPDATE;
Tarehe 15 March ndio uzinduzi rasmi, tutatembea kwa miguu wilaya zote 3 za Dar es Salaam tutaanzia Leaders Club, tutapita ilala na kuishia TCC Club chang'ombe.
Matembezi ya jioni ushawahi kuona? Kuanzia 10 kamili mpaka 12 jioni?
Tutaimba na wasanii wetu, tutawasha mishumaa zaidi ya 10000 kukumbuka albino wote waliouwawa bila hatia na hapo ndio mwisho wa matatizo utakapotangazwa rasmi.

Bloggers wenzangu (Tanzania Bloggers Network) wamejitoa kuwa waratibu wa hii shughuli, kwa hali na mali.

Dr. Magufuli atoa msaada wa kumuuguza mama wa albino


Mama wa mtoto mwenye ualbino Bi. Esther Jonas aliyekatwa mapanga akijitahidi kuokoa mtoto wake aliyenyanganywa na kuuwawa kinyama kisha kunyofolewa viungo vyake amekabidhiwa msaada wa shilingi milioni moja zilizotolewa na mbunge wa Chato Dr. John Magufuli kwa ajili ya kumsaidia wakati akiuguzwa hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza.
Bi. Esther Jonasi akipokea msaada wa fedha uliotolewa na Dr. Magufuli
                                                            

                                                                    Chanzo: ITV