Monday, November 3, 2014

Mungu mwenyewe awakemee wanaoitaka damu ya albino


Ninaukumbuka mstari mmoja wa Biblia, wakati malaika mkuu Mikaeli aliposhindana na shetani kuutaka mwili wa nabii Musa. Mikaeli alimwambia Mungu mwenyewe amkemee shetani kwa kuwa (Mungu) alikuwa na: Mosi, mamlaka juu ya mwili wa Musa, na Pili, alikuwa na uwezo kumzidi shetani. Maneno hayo yanasomeka hivi katika kitabu chaYuda 1:9;

"Lakini hata Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na shetani kuhusu mwili wa Musa, hakuthubutu kutamka hukumu juu ya shetani, bali alisema, “Bwana akukemee!”"
Hii inatokana na watu kuwa wagumu wa kuelewa, pia binadamu mwenzako ambaye si ndugu, wala haoni uchungu wa maumivu ya mtu albino hawezi kumtetea ipasavyo. Haiwezekani watu wanajiwekea matangazo ya jinsi ya kuwauwa albino kwenye mitandao kana kwamba wamepewa kibali cha kuwinda mbuga za wanyama. Hii sasa si sawa kabisa, kwa hakika Bwana Yesu mwenyewe awakemee!

Fikiri kijumuishi ~~ tenda kijumuishi ~~ jenga taifa jumuishi!