Saturday, September 20, 2014

Ajali za barabarani zinaongeza idadi ya watu wenye ulemavu



Mojawapo ya vyanzo vya mtu kuupata ulemavu ni pamoja na ajali anuai kwenye mazingira yetu. Mifano ya ajali  ni pamoja na zile za magari, pikipiki, kwenye michezo nk.


Tujitahidi kuweka mazingira mazuri kwa watu wenye ulemavu mbalimbali ili wasipate ugumu wa kuishi. Sheria, sera na mipango iwe jumuishi, majengo na miundo mbinu yote kwenye mazingira iwe rafiki kwa watu wenye ulemavu. Jambo kubwa kuliko yote ni kujiweka sawa kisaikolojia namna ya kuishi pamoja, kuwapokea kwa dhati na kuwahudumia watu wenye ulemavu.

Nimeshuhudia marafiki wengi ambao maisha yao yalikuwa mazuri na yenye kuvuta furaha, waliishi kwa kudhani ulemavu ni kwa jirani yake tu; lakini mara baada ya kupata ulemavu wamepotea kabisa kwenye ramani ya jamii. Waliokuwa wanasiasa imara hawavumi tena, waliokuwa na uchumi mzuri wameyumba, waliokuwa wanajihisi wanathamani kuliko watu wenye ulemavu kwa sasa wanajiona si binadamu. Hizi zote ni athari za kuwa na mtazamo hasi juu ya ulemavu na watu wenye ulemavu.

Hakika Mungu aturehemu na kutuhurumia!