Thursday, December 25, 2014

‘Sera kuhusu walemavu zipo, hazitekelezwi’

MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi yaUtafiti kuhusu Kupunguza Umaskini nchini (Repoa), Prof. Samwel Wangwe amesema sera zinazohusu watu wenye ulemavu zipo lakini hazitekelezwi.
Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kupokea tafiti iliyohusu namna wenye ulemavu wanavyoshirikishwa kwenye programu za mifuko ya hifadhi za jamii, Profesa huyo aliitaka serikali kuanza utekelezaji wa sera hizo sasa.
“Matokeo ya stadi hii tuliyofanya tutayapeleka serikalini kwa ajili ya utekelezaji… tunaishauri namna bora na sahihi ya kutekeleza sera hizo kwa kuwa wenye ulemavu nao wanaweza kuchangia pato la taifa kwa shughuli mbalimbali wanazofanya,” alisema Profesa Wangwe.
Fredrick Msigala ni mwakilishi wa wenye ulemavu kutoka CCBRT aliyeshiriki kufanya stadi hiyo kwenye baadhi ya wilaya hapa nchini alisema ni vema wakashirikishwa kutunga na kutekeleza sera zinazowahusu.
“Stadi hii imeona ni kiasi gani programu na mifuko ya hifadhi za kijamii zinawasahau wenye kuanzia kwenye namna ya kuwahudumia mpaka miundombinu ambayo sio rafiki kwetu.
“Tunaitaka serikali sasa itushirikishe wenye ulemavu tuweze kutunga sera kwa sababu matatizo yetu hayawezi kusemewa na mtu asiye mlemavu tunazo changamoto nyingi na sisi ndiyo pekee tunaoweza kuzisema sio mtu mwingine.
Stadi hiyo ilifanyika kwenye wilaya za Nachingwe, Muheza na Mbeya Mjini kwa ufadhili wa GIZ wakishirikiana na Repoa.

MFUKO WA GEPF WATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI




Meneja Masoko wa Mfuko wa GEPF, Bw. Aloyce Ntukamazina akiongea na vyombo vya habari juu ya mipango ya Mfuko huo kutoa misaada kwa jamii hasa kwa wale wenye mahitaji kama walemavu wa ngozi (Albino) katika shule ya matumaini ya Jeshi la Wokovu iliyopo Kurasini



Mtoto Maria Mwingira akipokea msaada wa mafuta maalum ambayo hukinga ngozi yao wakati wa jua kali kutoka kwa Meneja Masoko wa GEPF, Bw. Aloyce 


Ntukamazina.Kijana Salum Iddi akitoa neno la shukurani kwa Mfuko wa GEPF 




Watu wenye ulemavu tutumie siku hii kutafakari vizuri


Katika sikukuu hizi watu wenye ulemavu tutaona mengi
1. Tutakirimiwa
2. Tutaonyeshwa upendo na wengi
3. Tutaonyeshwa kwenye vyombo vya habari kuwa watu wanatujali
4. Nasi tutafurahi sana!

Lakini katika yote hayo sisi watu wenye ulemavu tutafakari mahali tulikotoka, mahali tulipo na mahali tunakokwenda. Hii itatusaidia kujiwekea mikakati ya kuondokana na utegemezi na kupunguza dhana ya kujiita na kuitwa wanyonge.


Kuwa imara, katekeleze likupasalo, hakika utafanikiwa!

Nakutakia sikukuu njema ya Christmas!