Monday, December 23, 2013

Je, Zitto Zuberi Kabwe bado anahitaji kubakia CHADEMA?

Mh. Zitto Kabwe awasili kwenye Viwanja vya Mwanga CENTRE na kutambulisho kwa viongozi wa chama, adai yeye (ZItto) ni Mbunge wa Kitaifa, Wanakigoma hawababaishwi na ubaguzi unaeondelea CHADEMA.

MWENYEKITI WA VIJANA MKOA WA KIGOMA ASEMA
Wanakigoma, ZItto ni mmoja wa vijana wa kigoma, tuna kila sababu ya Kumlinda, kumpigania na kusimama naye katika hatua zozote zile. Naomba tuungane kupambana naye kwenye hatua hii inayaoendelea ndani ya chama. Inauma sana kuona tumepigwa mabomu, risasi, tumetumia muda wetu kuijenga chadema, leo matunda yameanza kutoka wanakata mti kwasababu tu wao wanataka kujinufaisha. HAPANA!

KATIBU WA CHADEMA MKOA WA KIGOMA ASEMA
Nimeulizwa mwasali mengi sana kwanini hakuna bandera,kwanza ni salamu kwa Katibu Mkuu kuwa Chadema Kigoma hatuna bendera,fedha za kununulia hatua(ruzuku).Pia mapokezi ya zitto licha ya kuwa ya chama,ZItto tumempokea Kitaifa.

ZITTO KABWE APANDA JUKWAANI NA KUHUTUBIA
Nimekuja kuzungumza nanyi wanakigoma kwa Mujibu wa katiba ya chama,kama Katibu wa Mkoa alivyoeleza na katibu wa chadema hapa Kigoma mjini. 

Hivyo msithubutu kusikia propaganda zozote zile eti nitawajibishwa kwasababu ya kufanya mikutano nje ya Kigoma kaskazini,katiba ya chama inaniruhusu na katiba ya nchi inaniruhusu pia kwenda popote na kufanya chochote bila kuvunja sheria.

Wote mnakumbuka nilichukulia kadi kwenye uwanja huu mwaka 1993 nikiwa na miaka 16. Nimepata Ubunge nikiwa na miaka 29 kwenda kuwawasilisha wananchi wangu wa kigoma kaskazini na nchi nzima. Mnakubaliana nami namna nilivyokuwa kiongozi bora ndani ya bunge, Kuanzia hoja ya Buzwagi, Kumng'oa waziri mkuu na sasa Mabilioni ya Uswis.

Pia namna nilivyopigania ujenzi wa rami mkoa wa Kigoma, lakini lengo langu ni kutaka siku zote wanakigoma mjivunie kutaja kuwa wewe ni mzawa wa kigoma,na nimeshaijenga heshima hiyo.
Lakini ndugu zangu Ng'ombe akiumizwa malishoni anakimbilia zizini. Nimekuja Nyumbani kuzungumza na wananchi wangu, ndani ya chama nimeumizwa, nimevumilia sana kwa mikuki ninayopigwa na wenzangu ndani ya chama.

Uchaguzi wa ndani ya chama uliopita nilijitosa kugombea uenyekiti, lakini wazee wa chama wakaniita na kuniomba nimuachie mwenzangu awe mwenyekiti, NIKAKUBALI.

Lakini kuna vijana wamesulubiwa ndani ya chama kwasababu tu wamekuwa wakiniunga mkono. Mchange Habib alishinda uchaguzi wa Umoja wa Vijana, lakini matokeo yake yakafutwa na kupewa mtu mwingine wasababu yangu.

Akina Kafulila pia walishughulikiwa ndani ya chama kwasababu ya kudai haki, bahati mbaya sana Kafulila akaondoka chadema kwa hasira.

MIMI NITAPIGANIA HAKI YANGU kwa sababu ndani ya chadema kuna jasho langu, Kuna nguvu na mali zangu nilizopigania, Kuna watanzania waliopigwa risasi, mabomu na wengine kufariki kwasabau ya kupigania chadema.

KUONDOKA CHADEMA NI KUWASALITI WAPIGANIA HAKI, KUWASALITI WALIOKUFA KWASABABU YA KUIPIGANIA CHADEMA ISIMAME HADI HAPA ILIPO.

Pia naomba mtambue hoja yangu ya PAC inanimaliza chadema, Wenzangu ndani ya chama wananiandama kwasababu sikuwajulisha mapema kuhusu mahesabu ya ruzuku/mapato ya chama. Hakika katika hili nitaendelea kusimamia hoja yangu kwa Maslahi ya chama, Chadema lazima ikaguliwe kwa mujibu wa kanuni na sheria za nchi.

Jana mmesikia Slaa kwenye vyombo vya habari akisema atanifukuza eti vijana wanaoniunga mkono na wananchi wananiponza, Watanzania huku sio kufukuzwa?

Slaa ni katibu Mkuu wa chama na ndiye mwendesha vikao, leo hii anatoa huku kabla ya Vikao, huku sio kufukuzwa?

Mwenyekiti wa chama pia alinukuliwa na vyombo vya habari kule mwanza, eti zitto akirudishiwa vyeo vyake ndani ya chama labda mimi sio Mbowe! Wanzania huko sijafukuzwa tayari?

Leo hii wajumbe wa mkutano mkuu wameshaanza kuandikisha majina yao wakiomba mkutano mkuu uitishwe ili kujadili hatma ya mambo yanayoendelea ndani ya chama, pia kujadili rufaa yangu. LAKINI DR. SLAA ANAWATISHIA ETI WAOAFANYA HIVYO NI WASALITI NA WAHUJUMU WA CHAMA!


                                       Endelea kuangalia zaidi picha za mkutano huu.




Bendera ya CHADEMA haikupeperushwa kwa shamrashamra kama ilivyozoeleka kwenye mikutano mingi ya CHADEMA. Je hii ndiyo dalili ya kuwa watu walikwenda kumsikiliza Zitto kama Mwanakigoma na si kwa mambo ya kichama?

Dr. Nchimbi, Nahodha, na Kaghasheki wanastahili kushtakiwa


Kitendo cha kufanya uzembe kiasi cha kusababisha kuvunja haki za binadamu ni moja ya vigezo tosha kabisa mawaziri waliojiuzuru Tanzania kushtakiwa. Wananchi waliteswa na kuuawa kinyama.

Ili somo liwe limeiva ni vizuri hawa mawaziri wakashtakiwa kwa kosa hilo la kuvunja haki za binadamu.

Taarifa ya kamati ya bunge sehemu ya 2.2.4 inataja Changamoto za Operesheni Tokomeza kuwa ni pamoja na vifo vilivyotokea wakati wa Operesheni. Nukuu ya maneno ya taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kuhusu tathmini ya matatizo yaliyotokana na Oparesheni Tokomeza:
“Mheshimiwa Spika,Taarifa ya Serikaliiliainisha vifo kamachangamoto kubwa iliyojitokeza wakati wautekelezaji wa Operesheni Tokomeza kutokana na watumishi 6 na watuhumiwa 13 kupoteza maisha”.

Watu 13 walitajwa kama watuhumiwa, na ndio waliopata mateso makubwa na hatimaye wakafa kutokana na uzembe wa hawa mawaziri tajwa.


Baadhi ya wananchi walioteswa wakati wa operesheni

Mawaziri waliojiuzuru ni hawa hapa


Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kaghasheki


Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha


Waziri wa Mambo ya Ndani, Dr. Emmanuel Nchimbi

Zoezi la timuatimua kwa mawaziri lisiishie kwa hawa wanne tu (wa nne ni Mathayo David Mathayo). Nchi ina mambo mengi ya kuyafanyia kazi, wasipoweza kazi waondolewe ili kunusuru Taifa letu la Tanzania.

Kauli za Edward Lowasa ni nzito kama za mkuu wa nchi


Lowassa awapa matumaini bodaboda

JESHI la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani, lipo katika mazungumzo na waendesha bodaboda ili kuangalia namna ya kuimarisha usalama barabarani, na kupunguza vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu, vinavyofanywa na baadhi ya askari usalama barabarani kwa watu hao.
Hayo yalielezwa jana, wakati akizungumza kwenye tamasha la  Siku ya Waendesha Bodaboda Dar es Salaam (Bodaboda Day), lililofanyika katika viwanja vya Leaders na kudhaminiwa na Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) na Clouds Media Group.
Lowassa ambaye ni mbunge wa Monduli, alisema bodaboda ni ajira kwa vijana wengi waliokuwa mitaani, na hivyo ni vyema ikawa na mfumo rasmi, utakaowatambulisha na kuwasaidia kupata fursa mbalimbali za kiuchumi.
“Nimefanya mazungumzo na Mohamed Mpinga (Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani), na kuangalia ni namna gani ya kuwasaidia vijana wa bodaboda, amesema inawezekana, na sasa yupo katika mazungumzo na wadau wa bodaboda ili kuboresha usafiri huo.
“Kuna baadhi ya askari wa usalama barabarani ni wavunjaji wa sheria, wanaongoza kwa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu, lakini pia vijana wa bodaboda lazima waheshimu kazi yao kwa kufuata sheria ili kuifanya kazi hiyo iweze kuthaminika, na nawaahidi mkifuata sheria kama tulivyokubaliana, kila mmoja atapata pikipiki yake,” alisisitiza.
Alisema tatizo la foleni kwa Mkoa wa Dar es Salaam ni changamoto, na endapo bodaboda zikitumika vizuri, zitasaidia kupunguza adha hiyo na kuinua uchumi wa nchi.
Lowassa alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba asilimia 50 ya waendesha bodaboda si wamiliki, hivyo wanaandaa harambee itakayosaidia kuanzisha Saccos ili vijana wamiliki pikipiki zao binafsi.
Meneja wa Uchangiaji wa Hiyari PSPF, Mwanjaa Sembe, alisema wameamua kuwasaidia waendesha bodaboda na kuwaelimisha juu ya utamaduni wa kujiwekea akiba kwa maisha yao ya baadaye.
“Mafao yetu ni tofauti na mifuko mingine, na inawajali wafanyakazi wa serikali, sekta binafsi na hata mtu mmoja mmoja, sio tu bodaboda, lakini Watanzania wote wajifunze kuwa na utaratibu wa kujiwekea akiba,” aliongeza Mwanjaa.
Mmoja wa waandaaji wa tamasha hilo, Dennis Lucas, alisema nia ni kuunda umoja wenye manufaa, kwa kuelimishana na kutafutiana fursa, hususan kwenye mikopo, ili kuinua uchumi wa vijana nchini.