Monday, December 23, 2013

Dr. Nchimbi, Nahodha, na Kaghasheki wanastahili kushtakiwa


Kitendo cha kufanya uzembe kiasi cha kusababisha kuvunja haki za binadamu ni moja ya vigezo tosha kabisa mawaziri waliojiuzuru Tanzania kushtakiwa. Wananchi waliteswa na kuuawa kinyama.

Ili somo liwe limeiva ni vizuri hawa mawaziri wakashtakiwa kwa kosa hilo la kuvunja haki za binadamu.

Taarifa ya kamati ya bunge sehemu ya 2.2.4 inataja Changamoto za Operesheni Tokomeza kuwa ni pamoja na vifo vilivyotokea wakati wa Operesheni. Nukuu ya maneno ya taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kuhusu tathmini ya matatizo yaliyotokana na Oparesheni Tokomeza:
“Mheshimiwa Spika,Taarifa ya Serikaliiliainisha vifo kamachangamoto kubwa iliyojitokeza wakati wautekelezaji wa Operesheni Tokomeza kutokana na watumishi 6 na watuhumiwa 13 kupoteza maisha”.

Watu 13 walitajwa kama watuhumiwa, na ndio waliopata mateso makubwa na hatimaye wakafa kutokana na uzembe wa hawa mawaziri tajwa.


Baadhi ya wananchi walioteswa wakati wa operesheni

Mawaziri waliojiuzuru ni hawa hapa


Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kaghasheki


Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha


Waziri wa Mambo ya Ndani, Dr. Emmanuel Nchimbi

Zoezi la timuatimua kwa mawaziri lisiishie kwa hawa wanne tu (wa nne ni Mathayo David Mathayo). Nchi ina mambo mengi ya kuyafanyia kazi, wasipoweza kazi waondolewe ili kunusuru Taifa letu la Tanzania.

No comments: