Mauaji
ya ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi, yaani albino, ni ukatili usio na mfano.
Serikali haipaswi kuwa na huruma katika kuwasaka na kuwaadhibu wanaofanya
vitendo hivi. Ni muhimu pia kuweka utaratibu wa kuwalinda wenye ulemavu wa ngozi
dhidi ya tishio la kutekwa na kuuwawa. Elimu kwa umma ni muhimu. Wanaofanya
haya matendo wapo ndani ya jamii yetu. Tuweke utaratibu wa malipo kwa wasamaria
wema wanaotoa habari kuhusu wahusika wa biashara ya viungo vya binadamu. Na
tuweke utaratibu wa kuwalinda watoa habari hizi. Hili ni tatizo la kisheria
lakini pia ni tatizo la imani za ushirikina na uchawi ndani ya jamii. Ni lazima
kuyakabili mambo haya mawili kwa pamoja.
Albino
killings is a big shame. We must not tolerate this cruelty and animism. We must
hunt down the perpetrators and bring them to book. Tougher punishment is in
order but we have to first make it easier for perpetrators to get caught.
Public education is also a key. Perpetrators live amongst us. A reward scheme
and witness protection for those who reveal them could work. Effective policing
(security) too. This is a law and order issue (criminality) and also deeper
social issue - widespread belief in witchcraft. Must tackle both.
#TanzaniaMpya
#StopAlbinoKillings