Mtoto
Maimuna Yahaya (11) anayesoma shule ya msingi ya watoto wenye mahitaji maalum
(wenye ulemavu) ya Irente Rainbow (Lushoto- Tanga) darasa la pili, anasumbuliwa
na tatizo la mifupa na ukubwa wa kichwa tangu kuzaliwa kwake, tatizo
lililompelekea kuwa na ulemavu wa viungo na mtindio wa ubongo.
Mama
wa mtoto huyo, bi. Tunu Juma amesema amekuwa akimpeleka mwanae huyo Maimuna
katika hospitali ya KCMC kwa muda wa miaka 11. Hali ya mtoto inaendelea
kuimarika, anaweza kukaa na anaweza
kuongea. Bi. Tunu amekuwa akimpeleka mwanae huyu shule na kumsubiri hadi
wamalizapo masomo ya siku na kumrejesha nyumbani kwa muda wa miaka miwili.
Bi.
Tunu anasema kwa sasa hali yake ya kiuchumi si nzuri, anashindwa kumpeleka
mwanae kuhudhuria matibabu KCMC, hivyo anaomba msaada wa kifedha kwa wasamalia
wema ili mtoto wake aendelee na matibabu.
Mawasiliano:
Namba
ya simu ya mama mzazi: +255712504768
Namba
ya tigo pesa ya mtoto: +255655779345
Mahali
wanapopatikana: Lushoto Mabwawani