Waziri wa Fedha nchini, Dr. William Mgimwa amefariki dunia asubuhi ya leo baada ya kuugua maradhi ya presha kwa muda mrefu.
Taarifa zaidi zinasema Waziri wa Fedha William Mgimwa amefariki dunia leo katika hospitali ya Mediclinic Kloff nchini Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue, ambaye amesema Mgimwa amefariki majira ya saa 5:20 saa za Afrika Kusini ambapo ni sawa na saa 6:20 kwa majira ya Tanzania.
Naye January Makamba alonga namna alivyoguswa kuhusu kifo cha Mgimwa:
"Nimeumizwa sana na kifo cha Waziri wetu wa Fedha, Dr. Mgimwa. Alikuwa miongoni mwa wanasiasa wanyenyekevu na wanaoheshimu kila mtu. Alikuwa mzalendo wa kweli. Poleni sana familia yake, Poleni sana wana-Kalenga. Ametangulia, sisi sote tutamfuata. Mungu ailaze pahala pema peponi roho yake."
Source: Jamii Forum