Sunday, September 7, 2014

Rais Kikwete anatambua vizuri dhana ya ulemavu


Siku ya tarehe 9/7/2014, Mheshimiwa Rais J. M. Kikwete alitembelea Chuo Kikuu Cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU). Pamoja na mambo mengine aliyozungumzia, alisema wazi wazi na kwa tahadhari kubwa kuwa; "Ulemavu ni maumbile ya kawaida kwa binadamu, na watu wenye ulemavu wataendelea kuzaliwa."

Jambo la muhimu kwa yote ni serikali kuwezesha wanaharakati wenye uwezo wa kutoa elimu kwenye jamii juu ya dhana ya ulemavu na jamii. Watu wana dhana potofu juu ya ulemavu, na inafika mahali tunashuhudia ukatili wanaofanyiwa ndugu zetu albino.

Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na
mkuu wa wilaya ya Lushoto 
Bwana Majid Mwanga
Mhe. Rais Kikwete akiongea na jumuia ya SEKOMU
Makamu mkuu wa chuo cha SEKOMU, Dr. Aneth Munga akimkabidhi Rais kikombe chenye nembo ya SEKOMU
Wanafunzi wa shule ya wasioona ya Irente wakisoma risala kwa rais

Mhe. Rais Kikwete akizindua rasmi ukumbi wa mihadhara wa Benjamin Willium Mkapa SEKOMU