Ni kawaida ya binadamu atambuapo kuwa alifanya kosa lenye kugharimu nafsi za watu kwa namna moja au nyingine huomba msamaha. Uingereza waliomba msamaha kwa kuanzisha biashara ya utumwa; Papa kwa niaba ya Warumi aliomba msamaha kwa unyama waliomfanyia Bwana Yesu; Ujerumani waliomba msamaha kwa unyama waliowafanyia Wayahudi kwa kuwaua takribani milioni sita Wayahudi hao.
Je, kwa unyama ambao watu wenye ulemavu waliwekwa kwenye chemba ya gesi wakati wa utawala wa Hitler nani ataomba msamaha?
Je, unyama uliofanywa kwa watu wenye ulemavu kwenye "Eugenics Movements-the war against the weak" nani ataomba msamaha?
Je, ni nani mwenye ujasiri atakaye kuja mbele za watu na kuomba msamaha kwa mauaji ya albino nchini Tanzania?
Je, ni nani atakayethubutu kuomba msamaha kwa tamaduni kandamizi kwa watu wenye ulemavu?
Cheti cha uthibitisho kuwa mtu hana ulemavu. Watu wote waliokutwa na ulemavu waliuawa |
Tafadhali! Piga hatua moja tu ya kufikiri juu ya hili!