Ilikuwa ni shughuli ya kusafisha masikio, kutibu matatizo
madogo madogo ya masikio na kwa wale ambao ni viziwi walikuwa wakipimwa na
kisha kutengenezewa "shimesikio" earmould yaani umbile la sikio kwa
ajili ya kutengenezewa hearing aid. kazi hii ilikuwa inaendeshwa na wadhamin
toka Marekani "STARKEY HEARING FOUNDATION" Manesi na Madaktari toka
Sekoture pamoja na Walimu wanaofundisha watoto viziwi. Ilikuwa ni kwa watu wote
wenye shida ya masikio pamoja na viziwi wa hapa Mwanza. Tulianza siku ya ijumaa
tarehe 19/09 na kumalizika jumapili hii ya tarehe 21/09 hapa Nyanza S/M.
Mwl Fubusa (katikati) akiwa na wenzake tayari kwa kuanza upimaji wa masikio |
Mwl Fubusa akipima sikio la mwanafunzi |