Maana ya utamaduni
Utamaduni ni jumla ya
mambo yote yanayotengeneza na/au yanayounda maisha ya binadam. Utamaduni ndio
huwa kipimo cha kufikiri na kutenda. Utamaduni ndio hutufanya tutafsiriwe jinsi
tulivyo.
Utamaduni wetu huhusika
na maisha ya binadamu kiuchumi, kisiasa na kijamii. Chochote afanyacho binadamu
huongozwa na utamaduni, na hapa ndipo tunaweza kujipima kama utamaduni wetu
unatufaa au la.
Leo nazungumzia
utamaduni katika Nyanja ya uchumi. Kama nilivyotangulia kusema kuwa kufikiri
kwetu hutawaliwa na utamaduni tulionao. Vilevile mambo ya kiuchumi hutegemea
fikira za binadamu zilizotawaliwa na utamaduni.
Uchumi
wetu na watu wenye ulemavu (albino)
Miaka ya hivi karibuni
kumetokea kuwa na kundi dogo la binadamu ambao utamaduni wao kiuchumi lazima
wapate viungo vya albino. Kwa mtindo huu si rahisi sana kumbadilisha mtu
atafute utamaduni mwingine ambao hajauzoea. Maisha yao yote wanaamini mafanikio
na maisha mazuri kwao kiuchumi ni lazima wapate viungo vya wenzetu albino.
Ukiangalia kwa makini
utaona kuwa adui mkubwa wa ndugu zetu albino ni utamaduni wa jamii zetu. Imefika
mahali sasa tunapotambua kuwa utamaduni wetu tunaweza kuufananisha na mtu
aliyefuga mnyama akidhani ni mbwa kumbe ni simba, na huyu mnyama alivyoendelea kuwa mkubwa
ndipo alipojidhihirisha kuwa ni simba mla watu, na anajua mbinu zote za kumkamata
binadamu.
Ushauri wangu kwa
wanajamii wenzangu ni kwamba, tunatakiwa tubadili namna ya kufikiri, tubadilike
kimtazamo, tufahamu ubaya na uzuri wa tamaduni zetu. Tuwe wepesi wa kung’amua
mahali panapohitaji marekebisho kiutamaduni.
Watoto albino wakionyesha kufurahia mazingira yao.
Mama mzazi akiwa na wanae wawili ambao ni albino. Mwanamke yeyote anaweza akazaa watoto wakiwa albino.
Chanzo cha picha: http://24.media.tumblr.com/ccb063953efcb5113c5430005d53b5fe/tumblr_mjkddmFIQ31qhookmo1_500.jpg
http://www.scientificamerican.com/media/inline/killing-albinos-tanzania-albinism_1.jpg