Club Foot ni nini?
Hii ni aina ya ulemavu
utokanao na matatizo ya mifupa ambapo kunakuwa na mkao usio wa kawaida wa
unyayo wa mguu (unusual position of the foot).
Dalili za kuwa na “Club
Foot”
1. Unyayo waweza kuwa
mdogo kuliko ilivyo kawaida
2. Unyayo unaweza
kuinamia chini (kutembelea vidole)
3. Mguu (unyayo)
unaweza kuelekea ndani (turn in)
4. Ugumu wa kuvaa
viatu
5. Ugumu wa kushiriki
michezo itumiayo miguu (kwa watoto wakubwa)
Ulemavu huu mtu
anapata wakati gani?
Club Foot nyingi ni za
kuzaliwa (Congenitally Acquired), na nyingine hutokea wakati mtoto amezaliwa
katika hatua yoyote ya makuzi ambayo husababishwa na vigezo vya kimazingira tu
(environmental effects).
Ingawa Club Foot kwa
watoto haina maumivu, lakini taratibu za kitabibu zianze mapema mara mtoto azaliwapo
ili kupunguza athali zake kwa maisha ya kujitegemea baadae. Club Foot inaweza
kusababisha matatizo mbalimbali kadri mtoto anavyoendelea kukua, lakini
matibabu ya mapema humwezesha mtoto kuendesha maisha yake ya kawaida bila
kuhitaji msaada.
Nini husababisha mtoto
kupata “Club Foot”?
1. Mkao wa mtoto awapo
kwenye tumbo la mama yake (kabla ya kuzaliwa).
2. Mchanganyiko wa
athari za kiurithi (genetic factors) na za kimazingira (environmental factors)
ambazo kwa sehemu kubwa haziwezi kubainishwa kwa urahisi.
Athari kuu za “Club
Foot” kwa maisha ya mtoto
Uwepo wa “Club Foot”
kwa mtoto kunaweza pelekea matatizo mengine kama vile mfumo wa fahamu kupungua ufanisi
wake, ufanisi wa misuli mwilini hupungua; na pia mfumo wa mifupa nao hupungua
ufanisi wake kwa maisha ya mtoto.
Ushauri
1. Wamama wajawazito
wahudhurie kliniki kwa wakati ili kupata maelekezo muhimu kwa makuzi sahihi ya
mtoto awapo tumboni.
2. Wazazi wajawazito
wafanye mazoezi ya mara kwa mara (asubuhi na jioni) ili wawawezeshe watoto wao
tumboni kujiweka sawa (to make self adjustments in the womb)
3. Mara mtoto
akizaliwa na uonapo dalili dhahili za kuwepo kwa ulemavu wa “Club Foot” wahi
kwenye kituo cha afya kilicho karibu nawe ili upate ushauri wa kupunguza athari
za ulemavu huu.
4. Kwa vile “Club Foot”
ni moja ya ulemavu utokanao na matatizo ya mifupa; hivyo ni vema kama wana ndoa
wakashirikiana kwa karibu ili kuwezesha mtoto aliye tumboni kupata virutubisho
sahihi vya kujenga mifupa. Pata ushauri wa kitaalam wa lishe.
Mtoto mwenye Club Foot |
Upatapo elimu hii mshirikishe na mwenzako kwa ustawi wa familia zetu.