Miongoni mwa habari ambazo si wengi tunapenda kusikia ni kuhusu ulemavu na athali zake. Lakini leo napenda ujifunze kitu; kila jambo ulionapo linasisitizwa sana watu wajue athari na namna ya kukabiliana nalo "ujue kuna watu mahali fulani walipata athali fulani kwa sababu ya kukosa aina fulani ya maarifa kuhusiana na kitu fulani". Uzoefu unaonyesha kuwa ulemavu unaweza kumkabili mtu kwa hatua mbalimbali za maisha yake. Kwanza, kabla ya kuzaliwa (Mazingira au Urithi). Pili, wakati wa kuzaliwa (Mazingira). Tatu, wakati amezaliwa (Mazingira).
Ni habari zinazokereketa mioyo na fahamu za watu, sio nzuri kusikia; lakini ukweli unaonyesha kuwa familia zipatazo mtoto/mtu mwenye ulemavu huwa kuna mapito magumu sana hadi kuikubali na kuimudu hali hiyo kisaikolojia. Tumeshuhudia wazazi wakiwaficha watoto wao wenye ulemavu, wangine wakiripotiwa kuwauwa watoto wenye ulemavu mara wazaliwapo tu. Wababa wengine wameenda mbali zaidi kwa ama kutelekeza familia zao au kumkataa mtoto mwenye ulemavu aliyezaliwa.
Kujifunza na/au kuwa na taarifa sahihi kuhusu ulemavu, athali zake pamoja na uwezo wa kustahimili hali kutasaidia wengi wakati ikitokea wamepatwa na ulemavu. Nimeshuhudia wazazi wengi waliopata shida kwa kuzaa watoto wenye ulemavu. 1. Wanafuatilia waganga wa kienyeji wawape majibu ni kwa nini mtoto wao amezaliwa mlemavu (huwezi pata jibu huko). 2. Wengi wamepoteza fedha nyingi sana kwa matibabu hata kama ulemavu huo si wa kitabibu. 3. Wamekimbilia kwenye taasisi za dini ili waombewe, huku wakiukataa ulemavu kwa nguvu zao zote. 4. Hatimaye wanajiandaa kukubaliana na hali hiyo ya ulemavu, wanatafuta uzoefu kwa familia zingine zenye watoto wenye ulemavu.
Kwa hiyo uagundua kuwa kuna umuhimu wa kila mtu kuwa na ufahamu mzuri juu ya ulemavu ili iwe msaada wakati ukikutana na ulemavu au uweze kumsaidia jirani yako ambaye ni mlemavu au ana mtoto mwenye ulemavu.
Hata hivyo, kama Mungu amekujalia kupata uzee wema lazima ukutane na ulemavu wa macho au ukiziwi. Ndio maana mara nyingi utawasikia wazee wengi wakilalamika tatizo la macho, wengi wanapewa miwani.
Ni hamu yangu kuwa kila mtu aipate hii elimu, na ninaamini kuwa elimu kuhusu ulemavu itamfikia kila mtu kwa wakati wake uliokusudiwa. Tutapunguza athali za ulemavu kwenye maisha ya watu. Athali kuu ni kuharibika kisaikolojia kunakopelekea mtu kujiondolea thamani kwa binadamu wenzake, kufilisika kiuchumi, mchangamano mdogo na wanajamii wenzake nk. Fuatilia hili kwa makini, utagundua kuwa jamii/familia zenye watu wenye ulemavu zinadharauliwa sana na kunenwa vibaya.
Upofu |
Mwl na mwanafuzi wakiwasiliana kwa lugha ya alama ya viziwi |
Kipofu akitumia fimbo nyeupe |
NB: Ulemavu unaweza kumpata mtu awaye yote, katika hatua yoyote ya maisha, kwa mazingira yoyote, na muda wowote! (Every human being is a prime suspect for being attacked by disability).
No comments:
Post a Comment