Upo msemo mzuri wa kiswahili kuwa "ukitaka kuona mbali ni sharti usimame kwenye mabega ya mtu mrefu".
Siku zote watu wenye ulemavu wamekabiliwa na changamoto kemkem ambazo ziko ndani ya uwezo wetu. Watoto wengi wenye ulemavu wanakosa haki ya elimu kwa kuwa tu ni walemavu. Mfano; wapo watoto wasioona (blind), viziwi (deaf), na viziwi-vipofu (deaf-blind); hawa ni wengi katika jamii lakini wanashindwa kuifikia elimu kwa kigezo kuwa hakuna wataalam wa kuwafundisha.
Bado kuna kundi lingine la watu wenye ulemavu wa miguu, watu waliotakiwa wapewe magari ya matairi matatu (wheel chairs), lakini bado wengi wao hawana. Kundi hili linakabiliwa na miundo mbinu ya majengo ambayo si rafiki kwao.
Je, tumekosa watu warefu wa kuwawezesha watu hawa wenye ulemavu kuona mbali kimaisha? Tumeshindwa kuwawezesha wajitegemee? Je, nasi tusingewezeshwa kuona mbali tungekuwa tunafuraha ya kuishi leo?
Serikali itimize wajibu wake, na vikundi ya kijamii, na watu binafsi tuwekeze katika kuwasaidia watu wenye ulemavu ili nao wafanikiwe maisha yao, na pia wawe watu wenye mchango mkubwa kwa jamii yetu.
Mtu asiyeona akitumia kompyuta |
Mtu kiziwi-kipofu akielekezwa |
Uundaji wa teknolojia jumuishi kwenye usafiri |
Tufikiri juu ya hili!