Wednesday, December 25, 2013

RAIS JK ASHEHEREKEA KRISMASI NA YATIMA




RAIS Jakaya Kikwete amewakumbuka watu na watoto walio katika makundi maalumu kwa kuwapa zawadi kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Krismasi. Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii, Beatrice Fungamo alikabidhi msaada huo kwa niaba ya Rais Kikwete katika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo alitoa mchele kilo 1,150, ndoo za mafuta 11 za lita 20, ndoo ndogo nne za mafuta za lita 10 na mbuzi23.
Fungamo alisema msaada huo umetolewa kwa watoto yatima, wazee wasiojiweza na watoto walio katika mkinzano wa sheria katika vituo 17 nchini.
Alisema msaada huo aliokabidhi ni kwa vituo 11 vilivyoko Dar es Salaam ambavyo ni Kituo cha watoto IBN Kathir, Makao ya Watoto Kurasini, Makao ya Watoto Yatima Msimbazi, Kituo cha Yatima Group, Kituo cha Kwetu Mbagala Girls Home, Kituo cha Chakuwama, Mahabusi ya Watoto, Makao ya Watoto Yatima Mburahati, Vosa Mission, Kituo cha Tuwapende Watoto na Makao ya Wazee Wasiojiweza.
Alisema msaada kama huo umekwenda pia Pemba, Unguja, Kilimanjaro, Singida, Mwanza na Tanga.

CHANZO: GAZETI LA TANZANIA DAIMA

Pata Kazi Nzuri Hapa!

Sikukuu ya Krismasi yawa Faraja kwa watoto yatima Morogoro





Umekuwa ni utamaduni kwa Watanzania kuwakumbuka kwenye sikukuu watu wenye mahitaji maalum kama vile watu wenye ulemavu, watoto yatima na wale waishio kwenye mazingira magumu kimaisha.

Picha hizi ni za matukio ya miss Tanzania 2013 (Happiness Watimanywa) akiwa na watoto yatima wa kituo cha Magole, Morogoro
Miss Happiness Watimanywa akiwakabidhi zawadi watoto yatima
Wazazi wa Miss Happiness Watimanywa wakiwa wamembeba mtoto yatima
Miss Happiness Watimanywa na wadogo zake
wakiwa kwenye picha ya pamoja huku wakiwa
wamewabeba baadhi ya watoto yatima wa kituo cha Magole

Miss Happiness Watimanywa akitoa zawadi kwa watoto yatima


Rafiki wa Miss Happiness Watimanywa akiwa 
amembeba mtoto yatima wa kituo cha Magole