RAIS Jakaya
Kikwete amewakumbuka watu na watoto walio katika makundi maalumu kwa kuwapa
zawadi kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Krismasi. Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii, Beatrice Fungamo alikabidhi
msaada huo kwa niaba ya Rais Kikwete katika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo alitoa
mchele kilo 1,150, ndoo za mafuta 11 za lita 20, ndoo ndogo nne za mafuta za
lita 10 na mbuzi23.
Fungamo alisema msaada huo umetolewa kwa watoto yatima, wazee
wasiojiweza na watoto walio katika mkinzano wa sheria katika vituo 17 nchini.
Alisema
msaada huo aliokabidhi ni kwa vituo 11 vilivyoko Dar es Salaam ambavyo ni Kituo
cha watoto IBN Kathir, Makao ya Watoto Kurasini, Makao ya Watoto Yatima
Msimbazi, Kituo cha Yatima Group, Kituo cha Kwetu Mbagala Girls Home, Kituo cha
Chakuwama, Mahabusi ya Watoto, Makao ya Watoto Yatima Mburahati, Vosa Mission,
Kituo cha Tuwapende Watoto na Makao ya Wazee Wasiojiweza.
Alisema msaada kama huo umekwenda pia Pemba, Unguja,
Kilimanjaro, Singida, Mwanza na Tanga.
CHANZO: GAZETI LA TANZANIA DAIMA
No comments:
Post a Comment