Tuesday, April 17, 2018

TUJIFUNZE KUZUIA ULEMAVU USITOKEE

Image result for mama mjamzito 



Ulemavu unapatikana kupitia njia mbili tu
1. Kurithi
2. Mazingira

1. Ulemavu wa kurithi unaweza kuwa changamoto kuuzuia, japo mtu akifuata kanuni za kitabibu anaweza kuepuka. Mfano mmojawapo wa kuepuka hili ni kuepuka kuwa na ndoa na mtu wako wa karibu kiukoo (mtoto wa shangazi, mjomba, mama mdogo, mama mkubwa, baba mdogo, nk.)

Kabla ya kuoa / kuolewa onana na madaktari kwa ushauri wa mambo ya kiafya.

2. Ulemavu unaotokana na mazingira

Ulemavu utokanao na mazingira unajumuisha matukio yote yanayoweza kusababisha mtoto akazaliwa na ulemavu tangu kutungwa kwa mimba hadi kuzaliwa kwake huyo mtoto.

Baada ya kuzaliwa pia mtu anaweza akapata ulemavu kwenye mazingira yake ya kila siku.

Kama mama mjamzito, punguza uwezekano wa ulemavu kwa njia zifuatazo:
i. Pata lishe bora sawa na maelekezo ya madaktari.
ii. Hudhuria kliniki zote za kitabibu.
iii. Fuata maelekezo yote ya madaktari juu ya ujauzito.
iv. Pata kinga zote za kitabibu.

Baba mzazi jukumu lako ni:
i. Usimpige mkeo akiwa mjamzito.
ii. Usimfokee mara kwa mara mkeo mjamzito.
iii. Hakikisha mkeo mjamzito anapata lishe inayostahili.
iv. Mfanyie urafiki mkeo mjamzito ili kujenga maono (emotions) mema kwa mtoto.
v. Usimfanyie vitisho vyenye kuleta hofu na woga.
vi. Mpende mkeo mjamzito.


Baada ya kuzaliwa mtoto alindwe na hatari zozote hadi atakapokuwa na uelewa wa jema na baya kwa akili yake mwenyewe.

Uwe  na wakati mwema!