Monday, April 16, 2018

KUONGEZA THAMANI YA MTU MWENYE ULEMAVU

Image result for wajasilia mali wenye ulemavu 




Siku zote ulemavu huambatanishwa na matukio yote mabaya. Mtu mwenye ulemavu hufikiriwa kuwa ni masikini, asiyejiweza, naam, mtu tegemezi katika kila nyanja ya maisha ya mwanadamu. Hii dhana ni potofu, yafaa kukanushwa kwa nguvu zote, iwe kwa kuandika makala kwenye magazeti, kwenye vitabu, mihadhara, vipindi vya radio, tv na hata kwenye mitandao ya kijamii.

Hii dhana potofu kwenye jamii juu ya watu wenye ulemavu imeleta madhara katika mfumo wa maisha ya mtu mwenye ulemavu kwenye jamii. Moja ya madhara makubwa ni kuliona kundi hili ni jamii ya pili isiyo na thamani kwa kila kitu.

Njia za kuwaongezea thamani watu wenye ulemavu
1. Kuwafundisha watu wenye ulemavu kutumia vipaji vyao kujikwamua kiuchumi.
2. Kuwafundisha kujiamini
3. Kuwaeleza haki zao za msingi
4. Kuwachangamanisha na jamii nzima inayowazunguka.
5. Kuweka msisitizo wa elimu kwa watoto wote wenye ulemavu.


Tufikiri kijumuishi ~~ Tutende Kujumuishi ~~ Tujenge Taifa Jumuishi