WATU wenye ulemavu wa ngozi (albino), wamekuwa
wakisumbuliwa na maradhi ya ngozi hususan saratani ya ngozi.
Maradhi hayo hadi sasa, baadhi ya watu huyachukulia kuwa
labda hayana tiba, hiyo inatokana na jamii kuwatelekeza wapatwapo na maradhi
hayo. Jamii inapaswa kutambua kuwa maradhi hayo yana tiba
kinyume inavyodhaniwa na baadhi ya watu. Kutokana na mazingira hayo, serikali kupitia Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii imeweka mazingira mazuri ya kuwapatia matibabu watu hao
wenye wenye ulemavu wa ngozi. Mazingira hayo yatawasaidia albino kujikinga na ugonjwa
huo wa saratani ya ngozi, kulinda afya zao.
Rai kama hiyo imekuwa ikitolewa mara kadhaa na baadhi ya
wataalamu wa magonjwa hao. Miongoni mwa wataalamu hao baadhi yao ni madaktari
Bingwa wa magonjwa ya ngozi na afya ya jamii kutoka Hosipitali ya Rufaa ya
KCMC. Kauli kama hiyo waliwahi kuitoa wakati akitoa huduma kwa
walemavu wa ngozi katika Hospitali ya Mkoa wa Mwanza ya Sekou Toure kupitia
ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la Standing Voice.
Ushari huo unapaswa kufanyiwa kazi kwa sababu idadi ya
watu wenye ulemavu wa ngozi nchini ni kubwa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. Ieleweke kuwa maradhi ya saratani ya ngozi ni tatizo kwa
taifa hata hivyo, waathirika wakitibiwa mapema wanaweza kuepuka kupata kansa
hiyo.
Aidha, ni wakati kwa wadau na taasisi mbalimbali kuungana
kuwasaidia kimatibabu albino ambao
wanaonekana kupatwa na maradhi hayo. Kwa mfano kulikuwa na Shirika lisilokuwa la kiserikali
lenye makao yake makuu nchini Uingereza (Standing Voice ni), limewahi kufadhili huduma hiyo. Kipindi hicho shirika hilo liliamua kuwafadhili albino
waliokuwa wakishindwa kusafiri kufuata huduma hiyo katika Hospitali ya KCMC au
Ocean Road.
Tukubali kuwa tatizo hilo bado lipo na linazidi kukuwa
katika maeneo mbalimbali nchini, hivyo basi kila Mtanzania atumie nafasi yake
kuwasaidia watu hao wenye ulemavu wa ngozi.
Chanzo: Tanzania Daima