Elimu Maalum:
Hii ni taaluma ambayo mtu husomea, hususan, ualimu, ambapo hulenga kutoa taaluma na ujuzi maalum kwa makundi maalum kwenye jamii ili yaweze kuzifikia huduma mbalimbali kwenye jamii kama vile kupata elimu, kupata ajira, nk. Makundi haya maalum mfano wake ni watu wenye aina mbalimbali za ulemavu, watoto yatima, jamii za wafugaji na watoto wa mtaani. Ni wajibu wa kila taifa kuandaa sera nzuri zenye kutimiza mahitaji ya wanajamii wake.
Nchi yeyote na jamii yeyote ile lazima utawakuta watu wenye mahitaji maalum, na ambao kwa namna moja ama nyingine lazima lazima iwepo njia mbadala ya kuwapatia mahitaji kutokana na asili ya mahitaji yao. Hapa ndipo panaonekana umuhimu wa elimu maalum. Na kwa kuwa sheria na tamaduni za binadamu zinaonyesha kuwa kiumbe yeyote aliyezaliwa na/au kutokana na binadamu lazima aheshimiwe kama binadamu. Na pia katika makubaliano mbalimbali ya kimataifa kama vile Salamanca, Haki za binadamu za Umoja wa mataifa na mengine mengi yameainisha haki za msingi za watu wenye mahitaji maalum.
Mwl Rose Yona akiwasiliana na mwanafunzi kiziwi kwa lugha ya alama ktk shule ya viziwi Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Mwl Fanuel Mwakanosya akiwa ktk maandalizi ya kufundisha. Anatumia kifaa kiitwacho Perkins, mashine ambayo huweka maandishi ktk mfumo wa nukta nundu.
|
Mwl Magreth Msuya akitumia Perkins kuandaa nukuu za somo kwa wanafunzi wasioona wa shule ya msingi ya wasioona Buigiri mkoani Dodoma.
|
Mwl Magreth Msuya akimwezesha mwanafunzi wa darasa la sita somo la hesabu ktk shule ya msingi Buigiri.
|