Sunday, March 2, 2014

Afya ya Akili ni nini?





Tafsiri ya dhana ya afya ya akili

1.    Ni hali chanya kihisia na kisaikolojia inayomwezesha mtu kutumia uwezo wake wa kufikiri na kutawala hisia zake, katika kukabiliana na masuala mbalimbali ya kijamii, pia kuhimili changamoto mbalimbali za maisha ya kila siku.

2.    Uwezo wa kufurahia maisha, kujiamini, na kujikubali,  kuwakubali watu wengine, kujithamini na kuwathamini wengine, kuonyesha upendo na kuweza kupokea upendo kutoka kwa wengine, mawasiliano na ushirikiano mzuri kijamii, kuwajibika na kutekeleza majuku vizuri; ni mambo yanayoashiria kuwepo kwa afya bora ya akili.

Fikra, hisia na matendo ya mtu vinaashiria hali ya afya yake ya akili.
(Kwa mfano: Wewe unakabiliana vipi na msongo wa maisha?)
Mtizamo wako juu ya ubinafsi wako, mtizamo wako juu ya maisha unayoishi na unavyohusiana na wale uanoshirikiana nao katika maisha yako.
 Mfano: Je! Wewe unahusiana vipi na watu wengine?
Namna unavyopima njia kadhaa za kupata ufumbuzi wa suala lililo mbele yako.
 (Mfano: namna unavyofanya maamuzi katika maisha yako).

Nguzo muhimu kuhusu afya ya akili

  1. Fikra zako
  2. Hisia zako
  3. Matendo yako

Fikra zinazotawala mawazo yako


1. Mfumo wa kufikiri ni sehemu muhimu ya afya yako ya akili. Ni vizuri ukajitambua namna     fikra zako zinavyotafsiri masuala mbalimbali katika mazingira yako. (Kwa mfano: umekutana na rafiki yako akiwa na rafiki mwingine na inaelekea wanafurahiana na kucheka  pamoja)
2. Ni vizuri kujichunga aina ya mawazo yanayotawala fikra zako. Je! Unaruhusua fikra hasi    zitawale mawazo yako?
3. Fikra zinazotawala mawazo au ufahamu wako ni hutatawala mweleko wa hisia zako

          Hisia au namna Unavyojisikia

1.    Mzuka,   Furaha, Upendo, Utulivu, Amani
2.    Chuki, Wivu, Hasira, Wasiwasi, Woga, Huzuni

Wivu
Huzuni

Wivu




Huzuni



Mzuka






Hasira

Je! Unajisikia vipi? Tambua hisia zako

1.    Hisia ni sehemu muhimu ya ufahamu wa mtu kisaikologia. Fikra zako zinasababisha namna unavyojisikia. (Kwa mfano; ukigundua jengo hili linawaka moto …….)
2.    Iwapo Mawazo yahayotawa ufahamu wako ni hasi, utakuwa na hisia za wasiwasi, woga, pengine chuki and wivu.
3.    Ni muhimu kujitambua hisia zako. Mfano; Ninajisikia mwenye hasira, sina raha. Ni vizuri kujiuliza hii hasira inatoka wapi au inatokana na nini. Unafikiria nini kuhusu tukio fulani? Tukio la kawaida kwa watu wengine kwako linaweza kuwa na maana mbaya au hasi.
4.    Jiulize kama tukio husika linahalalisha wewe uwe na hasira au chuki.

Vitendo hutokana na mawazo na hisia zako.

Fikra zako zinaleta mabadiliko katika hisia zako, na hii inakuwa chimbuko la yale utakayotenda. Mifano; ………..

KUJIFUNZA KUTOKA MAISHA YA UTOTO

  1. Tangu utotoni tunajifunza kwamba matendo Fulani yana matokeo mabaya kwetu. Kwa mfano; Ukigusa kitu cha moto unaungua na kupata maumivu, au ukifanya kosa unaweza kuadhibiwa.
  2. Kwa mfano huo, ni vizuri pia tukajua kwamba fikra na hisia mbaya lazima zitakuwa na matokeo katika maisha yetu. Kama ni fikra mbaya zinazoambatana na hisia mbaya, matokeo yake nayo yatakuwa mabaya.
TAZAMA MIFANO MICHACHE

Hali ya afya ya akili huleta mabadiliko katika uhusiano na watu wengine
      Matatizo ya afya ya akili yanaathinri uhusiano na familia, ndugu, wapenzi, majirani, mwajiri, …….


Matatizo ya afya ya akili yanaweza kuathiri uwezo wako wa kukabiliana na masomo

  1. Inaathiri uwezo wa kufuatilia masomo kwa makini
  2. Inaathiri uwezo wa kutoa kipaumbele kwa masuala muhimu
  3. Inaweza kuathiri tabia na mwonekano wako darasani
  4. Uwezo wa kuweka mambo kwa mpangilio mzuri kubadilika
  5. Pia uwezo wa kujenga hoja na kuiwasilisha kwa ufasaha inaweza kuathirika.

Afya mbaya ya akili kama chanzo cha matatizo mengine:

  1. Kujaribisha dawa za kulevya
  2. Ngono  na wapenzi wengi kama namna ya kujiliwaza
  3. Kuwa mkorofi na mgonvi
  4. Kujiingiza katika tabia hatarishi

Namna ya kuimarisha afya ya akili

  1. Kula na kunywa maji ya kutosha
  2. Fanya mazoezi ya viungo angalau mara tatu kwa wiki
  3. Jali afya yako kila siku (jitambue na epuka vishawishi vya kula au kunywa vitu vinavyoathiri afya yako)
  4. Jipe muda wa kutafakari maisha yako mara kwa mara
  5. Muda wa kulala uwe wa kutosha – wastani wa saa 7 kwa siku
  6.  Chukua hatua madhubuti kukabiliana na dalili za msongo
  1. Kucheza au kushiriki matendo ya kujifurahisha – tafuta fursa za kujifurahisha kwa namna ambayo inajenga afya yako na kupunguza msongo.
  2. JITAMBUA – Fahamu na tawala fikra na hisia zako
      Unaweza kuanzisha daftari la kuweka kumbukumbu za fikra na hisia mbalimbali ambazo unaona ni muhimu katika maisha yako.
      Jitambue unapokuwa na fikra au hisia ambazo ni tofauti na kawaida yako
      Wakati mwingine unatakiwa kusema hapana kwa baadhi ya majukumu hasa pale yanapokuwa mengi mno kulingana na muda ulio nao.
      Tenga muda wa kutuliza akili yako, hakuna redio, TV na simu unaizima kukupa muda wa utulivu katika nafsi yako.


Nifanyeje kulinda afya yangu ya akili?

1.    Tambua dalili za mabadiliko:
      Namna unavyofikiri (aina ya mawazo yanayotawala akili yako)
      Katika hisia zako (unajisikia tofauti na kawaida yako – labda una wasiwasi, huzuni, au unapatwa hasira bila sababu kubwa)
      Unaonyesha matendo ambayo ni tofauti na kawaida yako
      Jifunze mbinu za kupunguza msongo wa mawazo na kuepuka tabia ambazo ni hatarishi kuleta msongo siku zote za maisha yako.
2.    Ni muhimu kujua ni lini na wapi unaweza kupata msaada iwapo utakuwa na msongo.
      Pata huduma mapema iwezekanavyo
3.    Pata huduma kutoka kwa mtaalam na pengine upate rufaa



ASANTENI KWA KUJIFUNZA