1.
Ni hali chanya kihisia na kisaikolojia
inayomwezesha mtu kutumia uwezo wake wa kufikiri na kutawala hisia zake, katika
kukabiliana na masuala mbalimbali ya kijamii, pia kuhimili changamoto
mbalimbali za maisha ya kila siku.
2.
Uwezo wa kufurahia maisha, kujiamini, na
kujikubali, kuwakubali watu wengine,
kujithamini na kuwathamini wengine, kuonyesha upendo na kuweza kupokea upendo
kutoka kwa wengine, mawasiliano na ushirikiano mzuri kijamii, kuwajibika na
kutekeleza majuku vizuri; ni mambo yanayoashiria kuwepo kwa afya bora ya akili.
Fikra, hisia na matendo ya
mtu vinaashiria hali ya afya yake ya akili.
(Kwa mfano: Wewe
unakabiliana vipi na msongo wa maisha?)
Mtizamo wako juu ya ubinafsi
wako, mtizamo wako juu ya maisha unayoishi na unavyohusiana na wale
uanoshirikiana nao katika maisha yako.
Mfano: Je! Wewe unahusiana vipi na watu
wengine?
Namna unavyopima njia kadhaa
za kupata ufumbuzi wa suala lililo mbele yako.
(Mfano: namna unavyofanya maamuzi katika
maisha yako).
Nguzo muhimu kuhusu afya ya
akili
- Fikra
zako
- Hisia
zako
- Matendo
yako
Fikra zinazotawala mawazo
yako
1. Mfumo
wa kufikiri ni sehemu muhimu ya afya yako ya akili. Ni vizuri ukajitambua namna fikra zako zinavyotafsiri masuala mbalimbali katika mazingira yako. (Kwa
mfano: umekutana na rafiki yako akiwa na rafiki mwingine na inaelekea
wanafurahiana na kucheka pamoja)
2. Ni
vizuri kujichunga aina ya mawazo yanayotawala fikra zako. Je! Unaruhusua fikra
hasi zitawale mawazo yako?
3. Fikra
zinazotawala mawazo au ufahamu wako ni hutatawala mweleko wa hisia zako
Hisia au namna Unavyojisikia
1. Mzuka, Furaha, Upendo, Utulivu, Amani
Je! Unajisikia vipi? Tambua
hisia zako
1. Hisia
ni sehemu muhimu ya ufahamu wa mtu kisaikologia. Fikra zako zinasababisha namna
unavyojisikia. (Kwa mfano; ukigundua jengo hili linawaka moto …….)
2. Iwapo
Mawazo yahayotawa ufahamu wako ni hasi, utakuwa na hisia za wasiwasi, woga,
pengine chuki and wivu.
3. Ni
muhimu kujitambua hisia zako. Mfano; Ninajisikia mwenye hasira, sina raha. Ni
vizuri kujiuliza hii hasira inatoka wapi au inatokana na nini. Unafikiria nini
kuhusu tukio fulani? Tukio la kawaida kwa watu wengine kwako linaweza kuwa na
maana mbaya au hasi.
4. Jiulize
kama tukio husika linahalalisha wewe uwe na hasira au chuki.
Vitendo hutokana na mawazo na hisia zako.
Fikra zako zinaleta mabadiliko katika hisia zako, na hii inakuwa chimbuko la yale utakayotenda. Mifano; ………..
Fikra zako zinaleta mabadiliko katika hisia zako, na hii inakuwa chimbuko la yale utakayotenda. Mifano; ………..
KUJIFUNZA
KUTOKA MAISHA YA UTOTO
- Tangu
utotoni tunajifunza kwamba matendo Fulani yana matokeo mabaya kwetu. Kwa
mfano; Ukigusa kitu cha moto unaungua na kupata maumivu, au ukifanya kosa
unaweza kuadhibiwa.
- Kwa
mfano huo, ni vizuri pia tukajua kwamba fikra na hisia mbaya lazima
zitakuwa na matokeo katika maisha yetu. Kama ni fikra mbaya zinazoambatana
na hisia mbaya, matokeo yake nayo yatakuwa mabaya.
TAZAMA
MIFANO MICHACHE
Hali ya afya ya akili huleta
mabadiliko katika uhusiano na watu wengine
•
Matatizo ya afya ya akili yanaathinri
uhusiano na familia, ndugu, wapenzi, majirani, mwajiri, …….
Matatizo
ya afya ya akili yanaweza kuathiri uwezo wako wa kukabiliana na masomo
- Inaathiri
uwezo wa kufuatilia masomo kwa makini
- Inaathiri
uwezo wa kutoa kipaumbele kwa masuala muhimu
- Inaweza
kuathiri tabia na mwonekano wako darasani
- Uwezo
wa kuweka mambo kwa mpangilio mzuri kubadilika
- Pia
uwezo wa kujenga hoja na kuiwasilisha kwa ufasaha inaweza kuathirika.
Afya
mbaya ya akili kama chanzo cha matatizo mengine:
- Kujaribisha
dawa za kulevya
- Ngono na wapenzi wengi kama namna ya
kujiliwaza
- Kuwa
mkorofi na mgonvi
- Kujiingiza
katika tabia hatarishi
Namna
ya kuimarisha afya ya akili
- Kula
na kunywa maji ya kutosha
- Fanya
mazoezi ya viungo angalau mara tatu kwa wiki
- Jali
afya yako kila siku (jitambue na epuka vishawishi vya kula au kunywa vitu
vinavyoathiri afya yako)
- Jipe
muda wa kutafakari maisha yako mara kwa mara
- Muda wa kulala uwe wa kutosha – wastani wa saa 7 kwa siku
- Chukua hatua madhubuti kukabiliana na dalili za msongo
- Kucheza
au kushiriki matendo ya kujifurahisha – tafuta fursa za kujifurahisha kwa
namna ambayo inajenga afya yako na kupunguza msongo.
- JITAMBUA
– Fahamu na tawala fikra na hisia zako
• Unaweza
kuanzisha daftari la kuweka kumbukumbu za fikra na hisia mbalimbali ambazo
unaona ni muhimu katika maisha yako.
• Jitambue
unapokuwa na fikra au hisia ambazo ni tofauti na kawaida yako
• Wakati
mwingine unatakiwa kusema hapana kwa baadhi ya majukumu hasa pale yanapokuwa
mengi mno kulingana na muda ulio nao.
• Tenga
muda wa kutuliza akili yako, hakuna redio, TV na simu unaizima kukupa muda wa
utulivu katika nafsi yako.
Nifanyeje
kulinda afya yangu ya akili?
1. Tambua
dalili za mabadiliko:
•
Namna unavyofikiri (aina ya mawazo
yanayotawala akili yako)
•
Katika hisia zako (unajisikia tofauti na
kawaida yako – labda una wasiwasi, huzuni, au unapatwa hasira bila sababu
kubwa)
•
Unaonyesha matendo ambayo ni tofauti na
kawaida yako
•
Jifunze mbinu za kupunguza msongo wa mawazo
na kuepuka tabia ambazo ni hatarishi kuleta msongo siku zote za maisha yako.
2. Ni
muhimu kujua ni lini na wapi unaweza kupata msaada iwapo utakuwa na msongo.
•
Pata huduma mapema iwezekanavyo
3. Pata
huduma kutoka kwa mtaalam na pengine upate rufaa
ASANTENI KWA KUJIFUNZA
No comments:
Post a Comment