Jambo la msingi kwa wanasiasa wanaojiandaa kugombea uchaguzi mkuu wa 2015 waje na ahadi kamili. Wasidanganye watu wenye mahitaji maalum. Tumeona mtu mmoja mwenye ulemavu akikutana na mwanasiasa na kupewa mlo mmoja tu hapo watatangaza kila media. Kila mtu anahitaji maisha bora bila kujali ulemavu wake. Wanasiasa njooni na ukweli ili kuinua maisha ya watu wenye mahitaji maalum, Halmashauri za wilaya na manispaa zimekalia fedha za watu wenye ulemavu, hawawapi haki zao.
Nitawaona wa maana sana kama mtawapa vifaa vya kuwawezesha kuendesha maisha yao wenyewe kama vile wheel chairs, artificial limbs, perkins machines, kuwapa mikopo na ruzuku, kuwajengea miundo mbinu bora nk. Tubadilike!
Wanafunzi wasioona |
Mtu kiwete aliyekosa wheel chair |
Mtu kiwete anategemea msaada wa kubebwa baada ya kukosa wheel chair |