Monday, September 15, 2014

Ahadi hewa kwa watu wenye ulemavu





Kila baada ya miaka mitano nchini Tanzania huwa kuna uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani. Hiki kipindi huambatana na maneno mazuri, na yenye kutia hamasa kwa watu wenye ulemavu. Wanasiasa hawa huenda mbali zaidi kwa kudhaminiwa na makampuni ya simu nchini ili kutuma ujumbe mfupi wenye maneno yenye ahadi kemkem kwa watu wenye ulemavu.

Jambo la msingi kwa wanasiasa wanaojiandaa kugombea uchaguzi mkuu wa 2015 waje na ahadi kamili. Wasidanganye watu wenye mahitaji maalum. Tumeona mtu mmoja mwenye ulemavu akikutana na mwanasiasa na kupewa mlo mmoja tu hapo watatangaza kila media. Kila mtu anahitaji maisha bora bila kujali ulemavu wake. Wanasiasa njooni na ukweli ili kuinua maisha ya watu wenye mahitaji maalum, Halmashauri za wilaya na manispaa zimekalia fedha za watu wenye ulemavu, hawawapi haki zao.

Nitawaona wa maana sana kama mtawapa vifaa vya kuwawezesha kuendesha maisha yao wenyewe kama vile wheel chairs, artificial limbs, perkins machines, kuwapa mikopo na ruzuku, kuwajengea miundo mbinu bora nk. Tubadilike!

Wanafunzi wasioona
Mtu kiwete aliyekosa wheel chair

Mtu kiwete anategemea msaada wa kubebwa baada ya kukosa wheel chair



No comments: