Vuguvugu la Eugenic lilianzishwa na Sir Francis Galton (mpwa wake Charles Darwin) mwaka 1883, likiwa na lengo la kuondoa kizazi kisichofaa duniani (dhaifu/weak people). Vuguvugu la Eugenic lilikuwa na lengo la kupiga vita watu wote waliokuwa na hitilafu kwenye miili yao. Watu wote wenye ulemavu waliingia katika kundi la watu wasiotakiwa kuishi. Kizazi chao kilitakiwa kupotea duniani.
Miongoni mwa mambo ya kukumbuka kwa vuguvugu hili ni:-
- Watu wote wenye ulemavu walidungwa sindano za kuwaondolea uzazi
- Adolf Hittler aliwatumbukiza watu wenye ulemavu kwenye chemba ya gesi kule Ujerumani na wakayeyuka kama maji.
- Watu wenye ulemavu hawakuwa na haki ya kuoa na/au kuolewa
- Watu wenye ulemavu walionekana si viumbe binadamu duniani
- Vuguvugu hili ndilo lililojenga utamaduni wa watu wenye ulemavu kunyanyapaliwa duniani kote.
Hivyo, tunapozungumzia athari za ulemavu hatuwezi kusahau mapito ya watu wenye ulemavu duniani kote. Tunapaswa kujua watu wenye ulemavu walikotoka, walipo na dira gani wanaelekea kwa nyakati za sasa.
Hakika, naam, wahenga walisema hakuna lenye mwanzo lisilokuwa na mwisho. Mwisho wa unyanyapaa huu upo; hata kama si mwaka huu basi hata karne zijazo.
Fikiri Kimapinduzi! Vunja kuta za unyanyapaa!