Siku zote ukikuta mwanamke au mwanaume amepata mwenzi mlemavu ujue huyo ni mwana mapinduzi. Kwanini tumwite mwana mapinduzi? Kwa sababu ameweza kupigana na kila aina ya fikra mbovu juu ya mwenzi wake mwenye ulemavu; amepokea kila aina ya laana juu ya uamuzi wake. Na mara nyingine hutokea wazazi wa mwenzi ambaye si mlemavu kumtenga ndugu yao katika familia na ukoo mzima kisa amempata mwenzi mwenye ulemavu.
Hili limedhihirika kwa mwanadada Mkenya aitwaye Salome aliyeamua kuoana na Solomon Kalube ambaye ni mlemavu wa viungo (hana mikono yote).
Salome alipoulizwa kwamba ni kwa nini aliamua kuolewa na mume mwenye ulemavu aliishia kwa kusema ni "ni uamuzi tu, na kwamba ulemavu si kutojiweza."
Hakika Salome amefikiri kijumuishi, ametenda kijumuishi, na amejenga taifa jumuishi!