Saturday, June 8, 2019

Habari za Ulemavu

...kila mtu mwenye ulemavu ana uzoefu fulani wa kupitia njia nyembamba ya kufanikiwa...

1. Ulemavu unaweza kumpata mtu yeyote, wakati wowote na mahali popote.
2. Usiwe kikwazo kwa mtu mwenye ulemavu. Kama humsaidii kwa lolote basi usimzuilie maendeleo yake..
3. Asili ya ulemavu ni sehemu ya haiba tu.
4. Binadamu aliyezaliwa na binanadamu ni binadamu tu; na ana haki ya asili kwa kuwa amezaliwa binadamu...
5. Usipime uwezo wa kufanya kazi kwa mtu mwenye ulemavu kwa kuhisi, kudhani, au kwa mihemko ya aina yeyote. Jipe muda wa kutosha kufanya uchunguzi...
6. (a)Wewe binafsi unamchukuliaje mtu mwenye ulemavu, mzazi mwenye mtoto mwenye ulemavu?
(b) Unadhani ulemavu ni wa watu fulani fulani tu?
(c) Unajisikiaje au unapata hisia gani ukikutana na mtu mwenye ulamavu?

Tushirikishane katika maisha haya yenye mrengo wa ushirikishaji...
Asanteni kwa kusoma ujumbe...

Image result for ulemavu wa macho
Mwanamke Msusi ambaye ni kipofu.