Biblia inasemaje juu ya ulemavu na watu wenye ulemavu?
Biblia ni kitabu cha
maandiko matakatifu ya Mungu. Ni muunganiko wa vitabu vidogovidogo vingi
vikipelekea jumla yake kuwa 66, agano jipya likiwa na vitabu 27, na agano la
kale likiwa na vitabu 39. Biblia ni kitabu cha pekee ambacho kimeathiri mtazamo
wa dunia nzima kuhusu masuala ya kalenda, mfano mtu akitaka kurejea tukio la
kihistoria lazima aonyeshe kama ni BK (baada ya Kristo) au KK (kabla ya
Kristo).
Katika mada hii
tutaangalia na kuchunguza maandiko matakatifu, hususan Biblia, inasemaje juu ya
ulemavu na watu wenye ulemavu.
Upofu (Visual Impairment)
Upofu (Visual Impairment)
Kwa mujibu wa Biblia Takatifu, upofu si dhambi wala laana; ni
mpango wa Mungu kuonyesha utofauti katika uumbaji wake. Katika huo ulemavu wa
macho ndipo na utukufu pamoja na nguvu za Mungu zinajidhihirisha (Yohana 9:1-3).
Nabii Musa ahojiana na Mungu kuhusu ulemavu wake
Nabii Musa ahojiana na Mungu kuhusu ulemavu wake
Kutoka 4:10-17, nabii Musa anatumwa na Mungu tayari kwa ajili
ya kazi ya kuwatoa wana wa Israel kule utumwani Misri. Musa alikuwa na ugumu wa
kuongea (Speech Impairment), na wakati anajitetea juu ya ulemavu wake na ugumu
atakaoupata kwa kazi aliyotumwa Mungu alisema maneno haya
“Bwana akamwambia, Ni nani aliyekifanya kinywa cha mwanadamu?
Au ni nani afanyaye mtu kuwa bubu au kiziwi, au mwenye kuona, au kipofu? Si
mimi Bwana?”
Yesu azungumzia kundi la watu wenye mahitaji maalum
Katika kitabu cha Luka 14:12-14; Yesu anazungumza kuwa
diakonia inatakiwa iwafikie watu wenye mahitaji maalumu, mathlani maskini,
viwete na vipofu.
Mambo ya Walawi 19:14, Biblia imeandikwa hivi:
“Usimlaani kiziwi, wala usitie kwazo mbele ya kipofu, bali
umche Mungu wako; mimi ndimi Bwana”.
*Neno Usimlaani, lina maana usimkatae au
usimtenge
*Usitie kikwazo, maana yake ni kwamba binadamu yeyote asimjengee
mazingira magumu ya kuishi binadamu mwenzake mwenye ulemavu.
Yesu amponya kiziwi
Yesu amponya kiziwi
Marko 7:32-37; Yesu anamponya mtu aliye kiziwi, anamwombea
kwa kuugua, anatumia neno Efatha.
Hitimisho
Hitimisho
Kama Biblia ambayo inaaminiwa na watu wengi kuwa ni kitabu
cha maandiko matakatifu, na ndicho kitabu kinachounda madhehebu ya Kikristo
yenye waumini wengi kuliko dini zingine dunia nzima, na iliyoathiri mtazamo wa
dunia kwa kiasi kikubwa huelezea vizuri
suala la ulemavu, kwanini sisi waumini wa hiyo imani tunaasi maagizo hayo? Kwa
waumini wa dini zingine wanaoheshimu maandiko matakatifu ya Mungu, kwanini
tunafanya mambo yanayoondoa ubinadamu wa watu wenye ulemavu?
Wote kwa ujumla, kama binadamu tunahitaji kuheshimiana,
kutendeana mambo mazuri, kutobaguana, kutonyanyapaana, na kuepuka mengine mengi
yenye kuondoa hadhi ya mtu kuitwa binadamu.
IMEANDALIWA NA SOKIME PHILEMON
No comments:
Post a Comment