Friday, February 28, 2014

Afya ya Akili Yako


“Burnout”
Kujisikia dhaifu / mchovu sana
kimwili na kiakili.

Mwili na akili kuishiwa nguvu ina maana gani?
(“burnout” ina maana gani?)
Hali ya kuishiwa nguvu mwilini, fikra na hisia kuwa za unyonge kutokana na kujituma mno kuliko uwezo  alio nao mtu. Mtu anajitoa sana kuwajibika au kuhudumia bila kujipa nafasi ya kupumzika.

Msongo unapozidi uwezo wako
1.     “Burnout” ni sehmu ya kukabiliana na hali ya msongo. Inatokea iwapo hali ya msongo inakuwa kubwa mno na kwa muda mrefu.
2.     “Burnout” ni hali ambayo inaathiri ufanisi wa mwili na akili.
3.     Mambo yanapokuwa magumu, mara nyingi tunasahau kujali na kulinda afya zetu. Tunaposahau kulinda afya zetu na kuruhusu hali ya msongo kutawala maisha yetu kwa muda mrefu, tunajiweka katika hatari ya kupata BURNOUT.

DALILI ZA “BURNOUT”
1.     Kimwili
2.     Akili /Hisia
3.     Mwenendo /matendo/


Mabadiliko mwilini
1.     Uchovu /kuishiwa nguvu
2.     Kukosa unsingizi au kulala sana
3.     Misuli ya mwili kukaza na kuuma
4.     Hamu ya kula kupungua au kuongezeka
5.     Maumivu ya kichwa
6.     Kupungukiwa tamaa ya kujamiana
7.     Kujisikia mgonjwa mwili mzima
8.     Mapigo ya moyo kwenda mbio.
9.     Dalili za shinikizo la damu
10.                        Tumbo kuchafuka / kuvimbiwa
11.                        Kupata vipele / kujikuna mwilini
12.                        Kupata mkojo mara kwa mara
13.                        Hali ya mchecheto na kutetemeka
14.                        Kupata mafua mara kwa mara


Mabadiliko kisaikolojia /hisia

1.     Feeling of loss of control
2.     Loss of meaning
3.     Feeling inadequate/incompetent
4.     Forgetful
5.     Resistant to suggestions
6.     Feeling trapped
7.     Difficulty concentrating
8.     Boredom
9.     Feeling work doesn’t fit in with personal values
10.                     Loss of sense of humor
11.                     In denial
12.                     Detached
13.                     Sad
14.                     Fearful/anxious
15.                     Frustrated
16.                     Overwhelmed

Mabadiliko ya mwenendo/ tabia

1.     Kupata ajali mara kwa mara
2.     Kukosa kazini mara nyngi kwa sababu za kiafya
3.     Pumzi ya kina mara kwa mara
4.     Kereka haraka /hasira za karibu
5.     Kutokwa machozi kwa urahisi
6.     Kujitenga
7.     Kutilia mashaka
8.     Mabadiliko katika uhusiano na watu wengine
9.     Kutojali kupuuzia
10.                        Kufanya kazi kwa bidii lakini ufanisi sana
11.                        Kuongezeka matumizi ya dawa, pombe na dawa nyingine kama za usingizi au za kulevya.

Ni nini chanzo cha “Burnout”?

Ø Masuala ya binafsi
Ø Matatizo yatokanayo na mazingira
Ø Masuala ya muundo /mfumo wa kazi

Masuala ya Binafsi

1.     Matatizo ya kiafya
2.     Kukinai /kuchoshwa na majukumu hali halisi
3.     Matatizo ya kifedha
4.     Mazoea ambayo hayana tija
5.     Kuhudumia bila “nafasi ya kupumua”
6.     Kukosa watu wa kutegemea /wanaokujali
7.     Mila na desturi /imani
8.     Ufinyu wa mikakati ya kisakolojia ya kukabiliana na changamoto za maisha
9.     Mahusiano ya usumbufu na kero

Matatizo ya mazingira

1.     Kelele, mwanga mkubwa, joto au baridi kupita kiasi, hewa nzito
2.     Msongo wa kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia /kukabiliana na taarifa nyingi mno kwa wakati mmoja
3.     Upungufu au kukosa vitendea kazi
4.     Mazingira hatarishi kazini
5.     Namna unavyokaa kwenye kiti /meza sehemu yako ya kazi
6.     Kuishi maisha ya kusongamana

Masuala ya mfumo au taratibu za kazi

1.     Kazi nyingi mno au kazi kidogo
2.     Majuku yasiyo wazi
3.     Majukumu mengi mno
4.     Kufanya kazi usiyo na ujuzi nayo
5.     Uwajibikaji
6.     Uwezo mkubwa mno kulingana na kazi, au uwezo mdogo
7.     Kutokujua usalama kazini utakuwaje baadaye
8.     Namna utawala unavyoendeshwa
9.     Utamaduni wa sehemu ya kazi
10.                     Mabadiliko ya mara kwa mara
11.                     Uwezekano mdogo wa kupata maendeleo, nafasi ya kuwa mbunifu au kuchangia

Namna ya kuikabili hali ya “Burnout”

1.     Chunguza na uondokane na zile sababu ambazo unafikiri zimekuletea hali ya “Burnout”
2.     Tambua yale ambayo yanawezekana kubadilisha na yale ambayo hayawezekani.
3.     Badili yale yanayowezekana
4.     Jiwekee malengo yanayoendana na yale unayothamini na kuamini kwa dhati.
5.     Weka mipaka iwe wazi kwako ni yapi yanawezekana au kukubalika na yapi hayawezekani.
6.     Wape wasaidizi wako baadhi ya majukumu
7.     Pumzika mara kwa mara, mazoezi, sala, mapumziko ya kutafakari
8.     Jiwekee changamoto mpya ambazo zinaendana na dhamira yako na ambazo zitakufurahisha.
Pata msaada kwingine

Namna ya kujikinga usifikie hali ya “Burnout”

1.     Jizoeshe kutawala akili yako, chunga fikra zako
2.     Pata mlo kamili unaokuongezea ufanisi
3.     Fanya mazoezi ya mwili angalau mara 3 kwa wiki
4.     Ukiona unachoka, jipumzishe
5.     Jifunze kuhimili changamoto za maisha, (kukubali, kufurahia unachofanya na uwe na shauku ya kukifanya vizuri)
6.     Jijengee tabia ya ucheshi na kufurahia ucheshi
7.     Jiwekee mazingira yanayoleta raha na kuchangamsha
8.     Epuka matumizi ya pombe au dawa za kulevya kama tiba ya “burnout”


Tunza akili yako kwa manufaa yako, familia yako, na jamii yako kwa ujumla wake!