KANISA KATORIKI KASULU WALIPOTEMBELEA KITUO CHA WALEMAVU KABANGA
Paroko,mwenyekiti wa kigango cha Murubona na Kumsenga pamoja na waumini
wengine wa Kanisa Katoriki Kasulu mjini,ahsantemi sana kwa kutembelea shule/kituo
chetu cha Kabanga na kutoa msaada wenu wa hali na mali na kubwa zaidi mchango wa
Tsh.1,700,000/=(Cash.Tsh.1,590,000/= pamoja na ahadi ambazo hutimiza jumla ya
kiasi tajwa hapo juu) kwa ajili ya mwanafunzi wetu Gilbert. Mbarikiwe sana ndugu zetu.
"MOYO USIO NA SHUKRANI HUKAUSHA MEMA YOTE"
|
Umati wa waumini wa Kanisa Katoriki Jimbo la Kasulu mjini walioambatana na Paroko lakini pia viongozi mbalimbali wa kanisa hilo kuja kuwajulia hali na kuwafariji walemavu wa ngozi(ALBINO) na kuwaletea zawadi kemkem siku moja kabla ya Pasaka (kwa kweli wamevunja rekodi haijawahi kutokea) kutembelewa na umati mkubwa kama huu. TUMEFARIJIKA SANA |
Baadhi ya wanafunzi na wakazi wengine waishio katika kituo cha walemavu Kabanga wakifurahia zawadi walizoletewa na waumini wa Kanisa Katoriki-Kasulu.(4.4.2015) |
Tufikiri Kijumuishi ~~ Tutende Kijumuishi~~ Tujenge Taifa Jumuishi