Friday, September 19, 2014

Haki ya elimu iko wapi kwa wilaya zisizo na shule za watoto walemavu?



Wanafunzi wenye mahitaji maalum wanapatikana kila mkoa, na kila wilaya ya Tanzania. Jambo moja ambalo nimeshangaa ni kuona baadhi ya wilaya nchini hazina shule kwa baadhi ya vitengo kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro; hakuna shule zenye kuwawezesha kupata mahitaji ya kielimu kwa watoto wasioona (blind), na watoto viziwi (deaf). Niliwahi kukutana na watoto wawili viziwi, nikawapeleka hospitali wakafanyiwa uchunguzi na kuonekana ni kweli ni viziwi. Nikafuata utaratibu wa sera ya elimu jumuishi, nikawapeleka wakaandikishwe shule, lakini hoja za walimu ni kuwa hakuna walimu wa kuweza kuwafundisha watoto hao viziwi.

Swali: Je, wilaya zenye matatizo ya shule za watoto wenye mahitaji maalum serikali haioni? Je, hawa watoto niliowapata, na wengine wengi ambao sikubahatika kukutana nao lakini wanauhitaji huo wa shule waendelee kukosa haki ya elimu?

Wadau tushirikiane na serikali ili kutatua hili tatizo!