Baby Madaha
Ni kwa sababu wananchi hawatoi ushirikiano unaotakiwa kwa wana-usalama, jambo linalosababisha kazi ya kuwabaini wauaji kuwa ngumu.
|
Coletha
Serikali haiwezi kushindwa kwa sababu wao ndiyo wenye kila kitu, polisi, jeshi usalama wa taifa na mahakama ni yao, sasa hapo wanashindwaje? Kama siyo udhaifu, tena wa makusudi dhidi ya wananchi katika utendaji kazi, wao ndiyo wenye wajibu wa kuwalinda wananchi wao.
|
Bi Mwenda
Wanawaonea sana, kwa kweli tangu wameanza kuwaua hakuna mabadiliko yoyote ya kimaendeleo waliyopata, pengine hata hao wanaopaswa kuzuia nao ni wahusika ndiyo maana kuna ugumu.
|
William Mtitu.
Mimi napendekeza atakayemkata mkono mmoja albino akishikwa akatwe mikono 2 na mguu mmoja ili iwe fundisho.Lakini pia itolewe elimu ya kutosha kuwa huwezi kutajirika kwa kiungo cha albino, kama kuna mtu anaamini anaweza basi aliyekamatwa na kiungo apelekwe baharini au ziwani avue samaki aone kama atavua samaki wengi, mahakama zitoe hukumu mapema zinapochelewesha maamuzi, ukatili na mauaji unaendelea.
|
Hussein Machozi
Serikali yenyewe ndiyo inawapa nguvu wauaji, na sisi inatufumba macho tu kuwa inawafuatilia. Rushwa kwa vyombo vinavyohusika na mauaji ya albino pia ni tatizo, serikali yenye nguvu ndiyo sababu ya hao wenzetu kufa mimi na wewe hatuna nguvu ya kuzuia hata robo.
|