Tuesday, February 24, 2015

Enzi za unyama zimerudia Tanzania




Zamani zile za biashara ya utumwa watu walitekwa na kupelekwa kusikojulikana! Walitenganishwa na familia zao kwa machungu.

Albino wanawindwa kama swala, kama sungura, wananyakuliwa kama vifaranga vya kuku mbele ya mwewe! Nina maumivu ya nafsi yangu na ya Watanzania wema wateswao kwa sababu ya hali ya ubinadamu wao.

Ninaendelea kusisitiza kuwa; wakishamalizwa hawa albino juu ya uso wa Tanzania watakaofuata ni binadamu wengine wenye ulemavu wa aina tofautitofauti, watu weupe, watu weusi, watu warefu, watu wafupi na wengine wengi wa aina nyingine ya haiba tofauti.

Napenda kuweka wazi kuwa watu wote wanaodhani kuwauwa albino ndio ushindi wa uchaguzi mkuu basi wamekosea mahesabu. Kwa sababu ya kilio cha damu isiyohatia ya hawa albino, natabiri anguko la wote wenye ushirikina huo!

Na alaaniwe kila amfikiriaye albino kwa nia mbaya ya kumwaga damu yake!
Watu wote na waseme amina...

Na alaaniwe kiongozi yeyote aliyeshinda uchaguzi mkuu kwa sababu ya kumwaga damu ya albino!
Watu wote na waseme amina...

Alaaniwe na asifanikiwe mtu awaye yote ambaye maisha yake yanategemea kumwaga damu ya albino!
Watu wote na waseme amina... 

Think Inclusively...Act Inclusively...Create an inclusive nation!

Albino wataka serikali ya Tanzania iwatafutie nchi ya kuishi kwa amani


JIJINI MWANZA, NCHINI TANZANIA, CHAMA WA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI MKOANI HUMO KIMEITAKA SERIKALI YA TANZANIA KUELEZA KAMA IMESHINDWA KUWEKA ULINZI JUU YAO, NA KUWATAFUTIA NCHI NYINGINE YA KUISHI AMBAKO HAKUNA MATUKIO YA KUTEKWA NA KUUAWA KWA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI. RAI HIYO WAMEITOA HII LEO WAKATI WAKITOA TAMKO LA KUTAKA KUJUA SERIKALI IMEFIKIA WAPI KATIKA KUWASAKA WALIOMTEKA MTOTO MWENYE ULEMAVU UPENDO EMMANUEL, ALIYETEKWA TAREHE 27.12. 2014 HUKO WILAYANI KWIMBA MKOANI MWANZA.

CHANZO: DW (Kiswahili)