Thursday, January 2, 2014

BENKI KUU YA TANZANIA (BoT) YATOA SARAFU YENYE THAMANI YA Tsh 50,000.



BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa sarafu maalumu ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye thamani ya sh 50,000. 

Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, a
lisema jana kuwa sarafu hiyo iliyotengenezwa kwa madini ya fedha kwa asilimia 92.50, imetolewa kwa ajili ya kumbukumbu tu na haitaingizwa katika mzunguko wala kutumika kwa kulipia malipo ya aina yoyote.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki ya BoT ilimnukuu Profesa Ndulu akisema sarafu hiyo imetolewa kwa idadi ya vipande 3,000 kwa ajili ya tukio hilo na kuwahimiza wananchi kuinunua kwa ajili ya kumbukumbu hiyo.

Kwa mujibu wa Gavana, kutolewa kwa sarafu hiyo kunakwenda sambamba na utaratibu wa Benki Kuu kutoa sarafu maalumu za aina hiyo kama sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya matukio mbalimbali muhimu ya kitaifa na kimataifa.

“Kwa kawaida, baada ya muda, thamani ya sarafu kama hizi huongezeka na kuwa na faida zaidi kwa wanaozimiliki,” alisema Profesa Ndulu.

Gavana Ndulu alieleza sarafu hizo zitapatikana Januari 5 kwa bei ya sh 50,000 katika matawi ya benki za biashara zitakazokuwa zimepata sarafu hizo kutoka Makao Makuu ya Benki Kuu, Dar es Salaam na matawi ya Benki Kuu yaliyoko Zanzibar, Arusha, Mbeya na Mwanza.

“Benki za biashara zinaweza pia zikasambaza sarafu hizi kupitia matawi yake,” alisema gavana na kuongeza taarifa za usambazaji zitatolewa na benki hizo.

Katika sarafu hiyo, upande wa mbele unaonyesha sura ya hayati Sheikh Abeid Aman Karume na maandishi yanayosomeka: ‘Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi’. Upande mwingine wa sarafu unaonyesha nembo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, maandishi yanayosomeka: “Miaka Hamsini ya Mapinduzi”, thamani ya sarafu na miaka 1964-2014.

SOURCE: Tanzania Daima

Je, Pingamizi La Zitto Mahakamani Kuzuia Kikao Kikao Cha Kamati Kuu CHADEMA inaashiria nini?



Zitto Kabwe ameweka pingamizi mahakamani kuzuia kikao cha Kamati Kuu kufanyika kesho.

Hoja yake ni kupinga kuitisha kamati kuu kabla shauri lake kusikilizwa na Baraza Kuu.

Anadai anataka mahakama iagize kamati kuu kutojadili suala lake mpaka baraza kuu likae kuamua rufaa yake.

Wanasheria wa Chama wakiongozwa na Tundu Lissu wanaenda Mahakamani kusikiliza pingamizi hilo ambalo litakuwa limeenda kwa hati ya dharura.

1. Wakili wa ZZK ni Alberto Msando.

2. Mawakili wa pande zote wapo Mahakamani.

3. Msando ndiyo ameruhusiwa kuanza kuwasilisha.

4. Jaji Utamwa ndiye anayesikiliza pingamizi hilo

ZZK amefikia uamuzi huo baada ya kupata taarifa za Mkutano Maalum wa Kamati Kuu ya chama kesho tarehe 3 Januari 2014 Jijini Dar Es Salaam. Ajenda kuu katika mkutano huo ni tatu;

Mosi; Kupokea taarifa kuhusu mchakato na maudhui ya mabadiliko ya katiba


Kamati Kuu itapokea taarifa juu ya kupitishwa kwa marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba 2013, kupitishwa kwa muswada wa kura ya maoni wa 2013, uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalum na kutolewa kwa Rasimu ya Katiba Mpya.


Pili; Kupokea utetezi (wa mdomo) wa wanachama watatu kuhusu tuhuma mbalimbali zilizoelekezwa kwao. 

Wanachama hao walishajulishwa makosa yao kwa maandishi na wamewasilisha utetezi wao wa maandishi. Wataitwa kwenye kikao kwa kuzingatia matakwa ya kanuni 6.5.2 (b) na 6.5.2 (d) kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.


Tatu; Mpango Kazi wa Chama kwa mwaka 2014 

Mpango Kazi wa chama ni sehemu ya hatua za utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Chama wenye dhima ya kuleta uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganizesheni thabiti kwa maendeleo endelevu ya chama na taifa.