Thursday, January 2, 2014

Je, Pingamizi La Zitto Mahakamani Kuzuia Kikao Kikao Cha Kamati Kuu CHADEMA inaashiria nini?



Zitto Kabwe ameweka pingamizi mahakamani kuzuia kikao cha Kamati Kuu kufanyika kesho.

Hoja yake ni kupinga kuitisha kamati kuu kabla shauri lake kusikilizwa na Baraza Kuu.

Anadai anataka mahakama iagize kamati kuu kutojadili suala lake mpaka baraza kuu likae kuamua rufaa yake.

Wanasheria wa Chama wakiongozwa na Tundu Lissu wanaenda Mahakamani kusikiliza pingamizi hilo ambalo litakuwa limeenda kwa hati ya dharura.

1. Wakili wa ZZK ni Alberto Msando.

2. Mawakili wa pande zote wapo Mahakamani.

3. Msando ndiyo ameruhusiwa kuanza kuwasilisha.

4. Jaji Utamwa ndiye anayesikiliza pingamizi hilo

ZZK amefikia uamuzi huo baada ya kupata taarifa za Mkutano Maalum wa Kamati Kuu ya chama kesho tarehe 3 Januari 2014 Jijini Dar Es Salaam. Ajenda kuu katika mkutano huo ni tatu;

Mosi; Kupokea taarifa kuhusu mchakato na maudhui ya mabadiliko ya katiba


Kamati Kuu itapokea taarifa juu ya kupitishwa kwa marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba 2013, kupitishwa kwa muswada wa kura ya maoni wa 2013, uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalum na kutolewa kwa Rasimu ya Katiba Mpya.


Pili; Kupokea utetezi (wa mdomo) wa wanachama watatu kuhusu tuhuma mbalimbali zilizoelekezwa kwao. 

Wanachama hao walishajulishwa makosa yao kwa maandishi na wamewasilisha utetezi wao wa maandishi. Wataitwa kwenye kikao kwa kuzingatia matakwa ya kanuni 6.5.2 (b) na 6.5.2 (d) kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.


Tatu; Mpango Kazi wa Chama kwa mwaka 2014 

Mpango Kazi wa chama ni sehemu ya hatua za utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Chama wenye dhima ya kuleta uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganizesheni thabiti kwa maendeleo endelevu ya chama na taifa.

No comments: