Diamond afunga mwaka 2013 na wakazi wa mkoa wa Lindi
Katika shamrashamra za kufunga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2014, hapo jana tarehe 31/12/2013, usiku wa kuamkia leo; palifanyika tamasha kubwa la burudani. Tamasha hili lilifanyika katika uwanja wa Ilulu mjini Lindi chini ya msanii wa muziki wa kizazi kipya, ndugu Nasib Abdul, alimaarufu kwa jina la 'Diamond Platnumz'. Lengo la tamasha hili mbali na kuukaribisha mwaka mpya, lililenga kudumisha Amani na Maendeleo jimboni Mtama.
Ni katika hekaheka za kuukaribisha mwaka 2014, ndivyo Diamond alivyotumbuiza huko mkoani Lindi |
Mbunge wa Mtama, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Benard Membe akipokea salamu za kuukaribisha mwaka 2014 kutoka kwa Diamond kwa niaba ya wana Lindi |
FM Academia Dar, ndani ya Business Park
Wanamuziki wa bendi ya FM Academia wakilishambulia jukwaa kwa show kali. Ni katika kuuaga mwaka 2013 |
Wanenguaji wa FM Academia wakiwa katika mapumziko |
Watangazaji wa Televisheni ya Taifa (TBC), wakiwa sambamba na FM Academia katika kuuaga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka 2014 |
Dar ndani ya uwanja wa burudani wa Dar Live
Mkoani Iringa, ndani ya Luxury Bari Iringa mambo yalikuwa hivi...
Tunawakakia Amani na Upendo Watanzania wote kwa mwaka 2014
No comments:
Post a Comment