Saturday, September 9, 2017

ULEMAVU WA MILANGO YA FAHAMU (SENSORY DISABILITY)

Image result for sensory disability


Huu ni ulemavu wa milango ya fahamu, yaani macho, masikio, pua, ulimi na ngozi. Asilimia 95 ya taarifa tuzipatazo kwenye mazingira zinatokana na milango ya fahamu. Hivyo, kwa kulemaa milango ya fahamu kuna athari za kimawasiliano kwenye mazingira ya binadamu.

1. Pua hainusi vizuri - Ulemavu wa kunusa
2. Macho hayaoni ipasavyo - Ulemavu wa upofu
3. Ngozi haihisi kitu - Ulemavu wa ngozi
4. Ulimi unashindwa kutofautisha ladha anuai - Ulemavu wa kuzungumza
5. Masikio hayasikii vizuri - Ulemavu wa kusikia

NAONGEA NA MZAZI/MLEZI



Kuna vifaa au vitu ambavyo unatakiwa uepuke kumwachia mwanao/mtoto wako avichezee. Kisu, msumari, kalamu ya wino, toothstick, na vifaa vingine vyenye ncha kali. Hivi vifaa vinaweza kuharibu macho na masikio ya mtoto akivichezea vibaya.

Vifaa vya kuchezea mtoto lazima viwe na usalama kwa mtoto.
 
No automatic alt text available.

Friday, September 8, 2017

Vuguvugu la Eugenic (The War Against the Weak)

Vuguvugu la Eugenic lilianzishwa na Sir Francis Galton (mpwa wake Charles Darwin) mwaka 1883, likiwa na lengo la kuondoa kizazi kisichofaa duniani (dhaifu/weak people). Vuguvugu la Eugenic lilikuwa na lengo la kupiga vita watu wote waliokuwa na hitilafu kwenye miili yao. Watu wote wenye ulemavu waliingia katika kundi la watu wasiotakiwa kuishi. Kizazi chao kilitakiwa kupotea duniani.
Miongoni mwa mambo ya kukumbuka kwa vuguvugu hili ni:-
  1. Watu wote wenye ulemavu walidungwa sindano za kuwaondolea uzazi
  2. Adolf Hittler aliwatumbukiza watu wenye ulemavu kwenye chemba ya gesi kule Ujerumani na wakayeyuka kama maji.
  3. Watu wenye ulemavu hawakuwa na haki ya kuoa na/au kuolewa
  4. Watu wenye ulemavu walionekana si viumbe binadamu duniani
  5. Vuguvugu hili ndilo lililojenga utamaduni wa watu wenye ulemavu kunyanyapaliwa duniani kote.
Hivyo, tunapozungumzia athari za ulemavu hatuwezi kusahau mapito ya watu wenye ulemavu duniani kote. Tunapaswa kujua watu wenye ulemavu walikotoka, walipo na dira gani wanaelekea kwa nyakati za sasa.
 
Hakika, naam, wahenga walisema hakuna lenye mwanzo lisilokuwa na mwisho. Mwisho wa unyanyapaa huu upo; hata kama si mwaka huu basi hata karne zijazo.

Fikiri Kimapinduzi! Vunja kuta za unyanyapaa!
 
Image result for eugenic movement

How negative perception affect people with disability


VIDEO: Ulemavu Si mwisho wa kuishi

                                                         
                                                           Jifunze kwa huyu dada!

LEO JITAMBUE WEWE NI NANI?


Majina yako ni haya:
1. Wewe ni jicho kwa wasioona
2. Wewe ni Sikio kwa viziwi
3. Wewe ni miguu kwa wasio na miguu
4. Wewe ni mikono kwa wasio na mikono
5. Wewe ni kila kitu kwa waliopungukiwa

NB: Mungu ni kila kitu kwako; naye anakutuma uwe kila kitu uwezacho kwa binadamu mwenzako!
Kutoka 4:11
"...ni nani afanyaye mtu kuwa bubu au kiziwi, au mwenye kuona au kipofu? Si mimi, BWANA?"

MCHANGA HULETA UPOFU WA MACHO



Moja ya sababu za kimazingira ambazo husababisha upofu ni mchanga. Ninao ushahidi wa mtu aliyepata upofu wa macho yake mawili kwa nyakati tofauti kwa kuingiwa na mchanga machoni.

1. Mwepushe mwanao asicheze sana kwenye mchanga
2. Angalia kwa makini aina za watoto wenye shirika na mwanao. Wengine ni wakorofi, wanaweza kuwaweka wenzao mchanga machoni
3. Omba Mungu kila siku akulindie mwanao!!!!
4. Kama una mlezi wa mtoto, angalia/chunguza tabia zake (huyo mlezi) ili kuelewa usalama wa mwanao
 
Image result for children playing on sands