KUZALIWA KWANGU KULETE MANUFAA KWA WENGINE |
Philemon Sokime (baba) na Jackline Sokime (mtoto) |
Mosi, namshukuru Mungu kuniacha nikiwa hai hadi siku ya leo
na kwa umri huu niliojaliwa naye. Kwa watu wa imani huamini kuwa kila jambo
mbele za Mungu lina makusudi yake, nami nakiri ya kuwa bado kuna jambo ambalo
Mwenyezi Mungu anataka nilifanye kabla sijatoweka humu duniani. Mengine yaweza
kuwa nayafahamu na mengine la.
Pili, naishukuru familia yangu ya msingi, yaani mke wangu “Magreth Mdendea Msuya” na mtoto wetu
mpendwa “Jackline Philemon Sokime”
kwa kunipa ushirikiano wa namna ya pekee wakati kwa wakati ufaao na usiofaa.
Wananishauri huku wakinitia moyo katika hatua mbalimbali ninazopitia.
Tatu, nachukua nafasi hii adimu kuishukuru familia yetu ya mzee
Ngiliule kwa kunilea hadi kufikia siku ya leo. Kwa taarifa tu ni kwamba “maisha
ya mtu ni matokeo ya maamuzi ambayo yalifanywa wakati uliopita juu yake, yaweza
kuwa ya wazazi, walezi/na au yeye mwenyewe”. Hivyo basi, maisha haya ya
kusoma na kupenda shule pamoja na jumla ya mazuri ninayofanya ni jumla ya maamuzi
ambayo wazazi wangu waliyafanya juu ya maisha yangu.
Nne, napenda kuwashukuru kaka zangu, dada zangu, wadogo zangu,
na wajomba zangu na ukoo mzima wa AKINA
KIGOSI ambao kwa ujumla wao na kwa
mtawanyiko wao popote walipo nchini. Wamekuwa msaada sana kwangu kwa hali na
mali. Wanapiga simu na wanapopata nafasi hunitembelea kwangu bila ya kujali
status walizonazo. Wamesoma na hawataki kuniacha nibaki nyuma kielimu. Tuko
pamoja sana.
Shukrani zangu za mwisho, napenda kuwashukuru ndugu wengine, jamaa na marafiki waliomo
nchini na wale walioko ng’ambo ambao kwa namna moja ama nyingine wamechangia
kuishi kwangu hadi siku ya leo. Nawapenda na tuko pamoja.
Zaidi ya hayo, napenda kuwajulisha wote niliowataja na ambao
sikuwataja kuwa, pamoja na mambo mengine mengi ambayo nimeyafanya, mojawapo
ambalo ni kubwa zaidi mbele za MUNGU na WANADAMU wenzangu ni kuanzisha huduma
ya utetezi kwa watu wenye ulemavu wa aina zote. Ninajua kuwa kazi hii ni ngumu,
inahitaji mtaji wa muda na fedha na pia OPRAS ya moyo. Huduma hii kwa sasa
inafanyika kupitia FACEBOOK na blog yangu changa iitwayo “SOKIME AND THE NEW INCLUSIVE NATION”
au www.sokime2012.blogspot.com .
Huduma hii inafanyika kwa maandiko ya kuwaelimisha watu juu
ya nini maana ya ulemavu, aina za ulemavu, chanzo cha ulemavu, utetezi kwa watu
wenye ulemavu na huduma zinazoweza kutolewa kwa mtu mwenye ulemavu ili
kupunguza athari za ulemavu kwenye maisha ya mhusika.
Natamani, napenda na ninaamini kuwa huduma hii kwa uwezo wa
Mungu itaweza kuvifikia vyombo vingine vya habari kama vile radio, magazeti na
TV. Pia naamini watapatikana watu wa kuniunga mkono kwa namna moja au nyingine
juu ya huduma hii ya namna yake.
Mwisho kabisa, ninawaomba msamaha watu wote ambao kwa namna
hii ama ile nilikuwa chanzo cha makwazo kwao, kuwasababishia hasara na usumbufu
wa namna tofautitofauti. Ninaamini hayo yote yalitokea tu kudhihirisha kuwa kwa
namna fulani naonekana kwenye jamii na kwamba uwepo wangu na kutokuwepo kwangu
mahali fulani kunaonekana wazi.
Katika siku yangu ya kuzaliwa, yaani tarehe 30/09 ni maombi
yangu kwa Mungu kuwa nyote mbarikiwe- Ibarikiwe siku niliyozaliwa; wabarikiwe wazazi walionizaa; wabarikiwe walionibariki na walionilaani; wabarikiwe wanaonikubali na wanaonikataa; wabarikiwe na maadui zangu pia.
TUFIKIRI KIJUMUISHI ~~~ TUTENDE KIJUMUISHI ~~~ TUJENGE TAIFA
JUMUISHI
HEBU TUJIKUMBUSHIE BAADHI YA MAANDIKO YANGU MACHACHE NILIYOWAHI
KUWEKA KWENYE MTANDAO:
THE
GREAT SECRETS OF DISABILITY
Disability is not a
disease, it is just like human diversity, and it differentiates one person from
the other. Furthermore, disability keeps an individual with disability or the
family having a member with disability speculating beyond the normal thinking body.
Through disability we come to see true friends and enemies, tolerant and
intolerant bodies, stoics and easy personalities; we get informed about how
people feel about disability. It is real that, through disability, human being
is assessed and screened about his/her personality. Through it, a long line
demarcation of perspectives is clearly drawn. In turn, individuals or families
having members with disabilities must have extraordinarily life styles for the
purpose of copping the emerging complexities within the diversified community.
In most cases, those great thoughts enrich the entire society by being informed
about the novel issues that are latent to human soul and his nature. Hence,
disability is the source of philosophy and logical means through which people
get knowledged about the nature of human being.
“To me, disability is
the hidden golden opportunity of the other side of the life in the Created
Socio-Cultural Universe, in which the Institute of Discovering the
Innate Human Sociological and Anthropological Vantages is of great deal”.
Sokime Philemon on the
Contemporary Disability Affairs -2013
DEVOTIONAL
WRITINGS
I will live
talking of Education, sleep dreaming of it, and once God takes me to his
heavenly palace- my educational devoted writings will speak on my behalf. This
is because, with education people get equipped with various knowledges of
socio-economic realms, political affairs, and the most important is that, it
helps human being review his nature.
“Sokime Philemon on the Contemporary Suitable
Education”.
2 comments:
Tupo pamoja my bro. Pendo simon
Pamoja sana Pendo! Naamini ipo siku tutafika tu hata kwa kutambaa na kwa machungu na magumu mengi. Hata hivyo tunatakiwa kufahamu kuwa ukweli wa leo si lazima uwe wa kesho. Nakumbuka habari ya rais wa zamani wa Marekani hayati John Kennedy alikuwa na dada yake ambaye alikuwa ana cognitive disability. Siku alipotembelelea kituo cha kulelea watu wenye ulemavu alikuta hali ni mbaya, watu wamejazana kama mifugo zizini, hakuna hata hewa nzuri, na wengi walitelekezwa na walezi wa vituo hivyo. Alichokifanya Kennedy ni kubadili sera za nchi ambapo hadi leo watu wenye ulemavu nchini Marekani maisha yao ni mazuri. Hivyo basi hata hapa kwetu Tanzania, ukweli na wakati vitaamua@Pendo Simon
Post a Comment