Tuesday, September 17, 2013

Omari Lubuva na mkakati wa kusaidia watu wenye mahitaji maalum

Bwana Omari Lubuva ni mtu asiyeona (blind). Ni mratibu wa TLB (Tanzania League for the Blind) mkoani Dodoma. Anahakikisha kidogo kinachopatikana kutoka kwa wasamalia wema kinawafikia walengwa. Endelea kuangalia matukio katika picha...


Ndg Omari Lubuva akimkabidhi bibi mchele
katika mkoa wa Dodoma eneo la miuji.




Vyakula vikiwa ndani ya mifuko tayari kwa kuwagawia
watu wasioona kwa ajili ya kujikimu kimaisha.


Watu haw wakifurahi baada ya kupewa chakula


Mzee wa miaka zaidi ya 80 ambaye pia haoni
amepata wasaa wa kumshukuru mwezeshaji
kwa kuwapa chakula hicho cha msaada.


Wabibi wawili hapa wakisikiliza kwa makini mgao
unavyokwenda. Wao tayari wameshapata cha kwao


Msoma ratiba ya mgao wa chakula akihakikisha
kama kuna yeyote aliyeachwa kwenye mgao huo

Ndg Lubuva akiwa na msoma ratiba ya mgao na mzee
wao mkongwe akiwasikiliza kwa karibu


Baada ya mgao wa chakula wanajiandaa kuondoka

Wanajamii hawa wanapata muda binafsi wa kumshuku
mwezeshaji wao kwa karibu. Wanaona ni kitu kigeni kwao


Wanaongoza njia kuelekea makwao



Fikiri Kijumuishi ~~~ Tenda kijumuishi ~~~ Jenga taifa Jumuishi



2 comments:

Anonymous said...

Tunatakiwa kumuunga mkono huyu jamaa Lubuva katika juhudi zake. Ni kweli watu wenye mahitaji maalum wanahitaji chakula na mahitaji mengine ya kimaisha.

Philemon Sokime said...

Ask any question, possible, humany, and wise answers will be sent to you!