Wakati Watanzania
wakifanya kumbukumbu ya miaka 14 tangu baba wa taifa , hayati J.K. Nyerere afariki
dunia hapo mnamo tarehe 14/10/1999; watu wenye ulemavu na wapenda haki za
binadamu wameendelea kumkumbuka. Aliwatetea sana watu wenye ulemavu, alirejesha
heshima ya binadamu na alijenga taifa jumuishi kupitia Siasa ya Ujamaa na
Kujitegemea iliyoainishwa kwenye Azimio la Arusha la mwaka 1967.
Mwalimu Nyerere pia anakumbukwa na wataalam wa mambo ya kielimu, ikiwemo elimu ya watu wazima, ambapo ilifika mahali kwamba kila kituo cha kazi kiligeuzwa kituo cha kisomo cha elimu ya watu wazima baada ya masaa ya kazi. Katika hotuba zake na maandiko mbalimbali kuhusu elimu alibainisha wazi kuwa elimu inatakiwa imwezeshe mtu kufikiri kimantiki na pia elimu hiyo itumike kama chombo cha ukombozi kwa mhusika (msomaji) na kumwezesha kujitegemea kwenye mazingira yake.
Nukuu za Mwalimu Nyerere:
Katika hotuba yake “Nguvu ya Walimu” aliyotoa Chuo cha Ualimu Morogoro, mwaka 1966, Mwalimu alisema yafuatayo:
“Taifa letu – taifa lolote – ni kubwa, ni zuri na mahali pazuri pa kuishi na kuendelea kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka na wanajitambua haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii. Na ukweli ni kuwa ni walimu, kuliko kundi lolote jingine ndio wanaoamua mtazamo huu, na kubadili mawazo na matumaini ya taifa”.
Desemba 1967 alisema:
“Mafanikio ya sehemu kubwa ya jaribio letu kujenga jamii ya kidemokrasia ni mkusanyiko wa mjadala huru kufuatiwa na utendaji wa maamuzi ya pamoja; kama watoto watazoea haya shuleni watakuwa wanajifunza majukumu ya uraia katika jamii huru.”
1976 alisema haya kuhusu elimu ya watu wazima;
“Jambo moja lisiloepukika ni kwamba lazima rasilimali zitengwe kwa ajili ya elimu ya watu wazima. Bila ya hivyo haitafanyika! Kupo kusisitiza katika wakati wa matatizo ya uchumi – jambo ambalo kwa nchi maskini ni la kila mara – kwa serikali kubana pesa kwa ajili ya elimu ya watu wazima. Na kuna tabia, pia wakati wa ukosefu wa wataalam, kuamua kuwa elimu ya watu wazima isubiri".

Na kuongeza kuwa:
“Elimu inayotolewa ni lazima ijenge mambo matatu kwa kila mwananchi, akili ya kuuliza, uwezo wa kujifunza kutoka kwa wengine - na kuyakataa au kuyakubali kutokana na mahitaji yake - na uwezo wa kujiamini kama raia huru na sawa katika jamii, anayethamini wengine na kuthaminiwa kwa anayofanya na siyo kwa anachopata”.
“Mafanikio ya sehemu kubwa ya jaribio letu kujenga jamii ya kidemokrasia ni mkusanyiko wa mjadala huru kufuatiwa na utendaji wa maamuzi ya pamoja; kama watoto watazoea haya shuleni watakuwa wanajifunza majukumu ya uraia katika jamii huru.”
Julius Nyerere, Elimu ya Kujitegemea alisema:
“Tulipoanzisha vyama vya wafanyakazi, na halafu baada ya Uhuru kwa uamuzi wa Serikali ya TANU, wafanyakazi wa Tanzania wamelindwa wasinyonywe na matajiri wao, watu binafsi, na hata mashirika ya umma. Na ulinzi huo umezidishwa siku hata siku. Kima cha chini cha mishahara kimewekwa na kimekuwa kikiongezwa mara kwa mara. Sasa ni vigumu sana kumfukuza mfanyakazi, na kila mfanyakazi apate heshima yake kama binadamu (Julius K. Nyerere (1974): UHURU NI KAZI, National Printing
Company Ltd, Dar es Salaam, ukurasa 15)”.
Company Ltd, Dar es Salaam, ukurasa 15)”.
1976 alisema haya kuhusu elimu ya watu wazima;
“Jambo moja lisiloepukika ni kwamba lazima rasilimali zitengwe kwa ajili ya elimu ya watu wazima. Bila ya hivyo haitafanyika! Kupo kusisitiza katika wakati wa matatizo ya uchumi – jambo ambalo kwa nchi maskini ni la kila mara – kwa serikali kubana pesa kwa ajili ya elimu ya watu wazima. Na kuna tabia, pia wakati wa ukosefu wa wataalam, kuamua kuwa elimu ya watu wazima isubiri".
1976: Katika mkutano wa Wakuu wa Shule za Sekondari, Dar es Salaam:
“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.”
WATU WENYE ULEMAVU NA RASIMU YA KATIBA YA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 2013:
Katika rasimu ya katiba mpya Tanzania, kuna vigezo ambavyo
vimemlenga moja kwa moja mtu mwenye mahitaji maalum (mwenye ulemavu). Vigezo hivi
vimeainishwa kama ifuatavyo:
Sura ya kwanza, sehemu ya kwanza, kifungu namba 4(3).
Serikali itaweka mazingira yatakayowawezesha kuwepo kwa
mawasiliano ya lugha mbadala zikiwemo lugha ya alama na nukta nundu kwenye
sehemu muhimu za umma na katika vyombo vya habari vitakavyotangaza habari zake
kitaifa kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum.
Sura ya 4, Sehemu ya Kwanza, kifungu namba. 44(1).
44.-(1) Mtu mwenye ulemavu anastahiki:
(a) kuheshimiwa, kutambuliwa nakutendewa kwa namna ambayo haishushi utu wake.
(b) kupata elimu kwa kutumia vifaa maalum na kushiriki katika shughuli za kijamii.
(c) kuwekewa miundombinu na mazingira yatakayowezesha kwenda anapotaka, kutumia vyombo vya usafiri na kupata habari.
(d) kutumia lugha za alama, maandishi ya nukta nundu au njia nyingine zinazofaa;
(e) haki ya kusoma na kuchanganyika na watu wengine; na
(f) haki ya kupata ajira na kugombea nafasi za uongozi katika nyadhifa mbalimbali kwa usawa.
(2) Mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha watu wenye ulemavu kushiriki katika nafasi za uwakilishi.zitakazomwezesha mtu asiyeona azitofautishe kwa thamani zake. Pia ni mategemeo yetu kuwa katika maeneo yote ya huduma muhimu za kijamii kama mabenki, taasisi za serikali pamoja na zisizo za kiserikali patakuwa na watafsiri wa lugha ya alama.
Hata hivyo, katika maoni
ya marekebisho ya mwisho ya rasimu ya katiba mpya ambayo Shirikisho la Vyama
Vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) lilifanya, lilipendekeza kuwa kila
mahali panapoainishwa makundi ya jumla ya watu, ni vizuri wakataja moja kwa
moja na watu wenye mahitaji maalum. Wadau wa elimu wanakumbuka suala la elimu
enzi za ukoloni; mahali walipotaja neno “wanafunzi” lilimaanisha wanafunzi wa
kiume tu. Baada ya uhuru wa Tanganyika mwaka 1961, wadau wa elimu walikuja na pendekezo
kuwa kila panapotajwa wanafuzi pia iongezwe maneno yaliyomaanisha “wa kiume na
wa kike” ili kupoteza dhana ya utengaji. Hivyo, SHIVYAWATA limetaka rasmu ya katiba
mpya ibainishe wazi hayo makundi ya watu kuwa ni pamoja na ya watu wenye
mahitaji maalum.
Hitimisho
Ni heshima kubwa tunayotakiwa kumpa huyu muasisi wa taifa la Tanzania kwa vitendo. Tujifunze kwa kadri alivyosema na akaishi kwa maneno yake aliyoyasema. Alifanya mengi kwa faida ya taifa ili kujenga misingi ya jamii imara na jumuishi kupitia elimu. Wakati huu kuelekea kupata katiba mpya ndio muda muafaka wa kumuenzi Mwalimu Nyerere.
Kuwa na katiba nzuri inamaanisha kuainisha vipaumbele vya wananchi ambao ndio msingi wa katiba yenyewe, na ambavyo wamevipendekeza wenyewe. Pia tunatakiwa tuitekeleze katiba yetu kwa vitendo. Mahali palipotajwa watu wenye mahitaji maalum na kipaumbele chao ni vizuri kikatekelezwa kama kilivyoainishwa. Mathalan, kwenye kipengele cha usawa wa upatikanaji wa habari kupitia vyombo vya habari, tunategemea kuona magazeti yanatolewa nakala za nukta nundu, sarafu na noti za fedha ziwe na alama.

“FIKIRI KIJUMUISHI ~~~
TENDA KIJUMUISHI ~~~ JENGA TAIFA JUMUISHI”
No comments:
Post a Comment