Kwa muda mrefu kumekuwepo na taarifa za
ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu; tumesikia walemavu wa ngozi (Albino) kwa
namna walivyofanyiwa na wanavyoendelea kufanyiwa ukatili kisa eti Imani za
kishirikina. Pamoja na yote uliyosikia lakini hebu fuatilia kisa hiki, ambapo
mlemavu asiyejiweza kabisa anavamiwa, anabakwa, anapewa Mimba, mwisho wa siku
anajifungua, lakini baada miaka kadhaa mwanaye aliyemzaa akiwa mzima naye
ghafla anakuwa mlemavu.
Tangu nchi yetu ipate Uhuru waka 1961
Serikali kupitia Idara ya Ustawi wa Jamii imekuwa inatoa huduma kwa watu wenye
ulemavu bila kuwa na sera timilifu.
Mary Petro, akiwa amepumzika |
Kuwapo kwa Sera ya Taifa ya Maendeleo
na Huduma kwa Watu wenye Ulemavu ni matokeo ya miaka mingi ya majadiliano baina
ya Serikali na wadau. Pamoja na kutokuwapo kwa sera, Tanzania imekuwa
inajihusisha na mipango mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa inayohusu masuala ya
ulemavu.
Kimataifa Tanzania imesaini mikataba
mbalimbali kuhusu watu wenye ulemavu hususan mikataba ya Haki kwa watu wenye
Ulemavu (1975), Haki za Mtoto (1989) na Haki na Fursa sawa kwa Watu wenye
Ulemavu (1993).
Barani Afrika, Tanzania ni miongoni mwa
nchi waasisi wa Mpango wa utekelezaji wa muongo wa Watu wenye Ulemavu na
mwanachama wa Taasisi ya Marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu (African
Rehabilitation Institute – ARI).
Hapa nchini serikali imechukua hatua
kadhaa ikiwa ni pamoja na kampeni za chanjo ya kuzuia ulemavu utotoni (kwa
mfano polio), kutunga sheria zinazolinda maslahi na kuboresha maisha ya watu
wenye ulemavu, kuwapo kwa swali kuhusu ulemavu katika sensa ya Taifa ya watu na
makazi (2002) na ile ya mwaka jana (2012) na mandalizi ya kuridhia
mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki na Fursa Sawa kwa Watu wenye Ulemavu.
Sera inatoa mwongozo na inaweka vigezo
vya utoaji huduma. Sera imejengwa kwa kuzingatia utamaduni wetu na inalenga
katika kuleta maendeleo, haki na heshima kwa Watanzania wenye ulemavu.
Changamoto iliyopo ni kutafsiri kwa
vitendo matumaini yaliyomo kwenye Sera hiyo na kilichopo tu ni kwamba kundi
hili limekuwa likikumbukwa pale tu linapotokea janga au unyanyasaji fulani na
baada ya hapo hakuna tena atakayejali na kulitilia maanani,kwani kukosa kwao
huduma mbalimbali za jamii, kunawafanya walemavu waathirike kisaikolojia na
wengi wao kukata tamaa ya maisha.
Pamoja na jitihada hizo za serikali
lakini bado kuna ukweli usiopingika kwamba kuna baadhi ya walemavu ambao
serikali haijawafikia mahali walipo, lakini kibaya zaidi hata jamii yenyewe
inayowazunguka haijaona umuhimu wa kuwatolea taarifa mahali husika.
Miongoni mwa watu wenye ulemavu ambaye
anaonekana wazi kwamba yuko katika hali ngumu huku serikali ikiwa haijui
taarifa zake lakini kibaya zaidi jamii nayo ikionekana kumtenga na kutomjali ni
Mwanamke Mary Petro (51) mkazi wa kitongoji cha Sima kijiji na kata ya Bupandwa
wilayani Sengerema Mkoani Mwanza.
Mary Petro: Ulemavu wake ni miguu na mikono |
Mlemavu huyo ambaye hana uwezo wa
kutembea,huku akiwa ni mtu mwenye kubebwa na watu wawili wakati wowote
anapotaka kufanya jambo lolote ikiwa ni pamoja na kwenda kujisaidia haja kubwa
ama ndogo,kula chakula mwenyewe kwa kutumia mikono yake miwili hilo ni jambo
ambalo halijawahi kumtokea tangu azaliwe miaka 51 iliyopita.
No comments:
Post a Comment