Ulemavu ni sawa na mtu kujikuta amezaliwa akiwa kabila fulani, akiwa na rangi fulani, akiwa mrefu au mfupi. Hakuna wa kumlaumu wala kujilaumu. Lakini kubwa zaidi ni kwamba dhana ya ulemavu imejengwa na jamii tu. Mitazamo yote imezalishwa na vitendo vya wanajamii.
Hivyo tunahitaji kuwa na mitazamo mizuri juu ya ulemavu na watu wenye ulemavu; kwa kuwa hatujui ni nani, na wakati gani atazaliwa na ulemavu, au atapatwa na ajali yenye kuleta ulemavu. Kuwa na mtazamo mzuri juu ya ulemavu na juu ya watu wenye ulemavu ni silaha ambapo muda wowote unapokutwa na ulemavu uweze kujikubali kwa hali, pia na watu wengine kwenye jamii waweze kukukubali na kukusaidia kwa yale utakayokuwa huwezi kuyafanya kwa sababu ya ulemavu.
Mtoto mdogo kiziwi akifundishwa lugha ya alama |
Mwenye masikio na asikie ujumbe huu!
No comments:
Post a Comment