MASHAKA AMINI HOSSEN ni mtoto mwenye ulemavu. Taarifa zake ni hizi hapa:
Aina ya ulemavu: Kiziwi (Deaf) na Ububu (Dump)
Umri: Miaka 9
Mahali alipo: Mtaa wa Mangedere
kijiji cha Kichangani, Turiani
mkoa wa Morogoro, Tanzania.
Wazazi wa MASHAKA AMINI ni wakulima wa kipato cha chini, hawamudu kumhudumia mtoto wao kwenda shule ya viziwi. Hitaji kuu la mtoto ni kutafutiwa shule ya watoto viziwi na kusomeshwa.
Mawasiliano:
Baba mzazi- +255714679645
Mwalimu Philemon Sokime: +255655410031/+255766750941/sokime2012@gmail.com
Mzazi wa mtoto MASHAKA AMINI anawaomba wasamaria wema waweze kumsaidia kitaalam na kifedha ili mwanae aweze kusoma shule za viziwi ndani ya Tanzania. Tatizo linalomkabili huyu mtoto MASHAKA AMINI ni kukosa shule iliyo jirani na huku wilaya ya Mvomero. Wilaya hii haina shule hata moja kwa ajili ya wanafunzi viziwi. Mtoto aliwahi pelekwa shule ya msingi Kichangani mwaka 2012 lakini walimu walishindwa kumfundisha kwa kuwa hawana utaalam wa elimu maalum.
Wadau wote wa elimu yatupas tufikirie namna ya kutatua tatizo hili kwa mtoto MASHAKA AMINI ili aweze kuelimika na baadae kuondoa utegemezi usio wa lazima.
Mwl Philemon Sokime akiwa na mtoto MASHAKA AMINIkatika mitaa ya soko kuu la Kichangani, Turiani |
AMINI akiwa na jirani yake mitaa ya sokoni |
Mwl Philemon Sokime yuko na MASHAKA AMINI |
MASHAKA AMINI akifurahia madhari yake! |
MASHAKA AMINI akiigiza kuuza vyombo! |
MASHAKA AMINI akifurahia gari la kuchezea watoto alilomnunulia mwalimu Philemon Sokime |
2 comments:
Kweli elimu ni haki ya kila mtu
Ni kweli ndugu yangu Amasha Kigosi. Elimu kwa sasa ndiyo kila kitu kwa maisha ya binadamu. Tunatakiwa kuhakikisha kila binadamu anapata hii haki ya elimu ili kuondokana na utegemezi usio wa lazima!
Post a Comment