Kila ustaarabu katika historia ya maisha ya mwanadamu huwa na eneo ambalo umeanzia.
Katika historia ya Elimu Maalum kwa vyuo vikuu imeanzia SEKOMU. Nakumbuka topic ya "Advocacy for people with disabilities". Zipo nadharia mbalimbali zinazohusu ulemavu, mojawapo ni ile iitwayo "Social Disability" ambayo inadai kuwa duniani hakuna kitu kinachoitwa ulemavu wala mtu mwenye ulemavu bali ni tafsiri iliyoundwa kwenye jamii ili kuwabagua binadamu wengine. It is a social constructed concept!
Pia nakumbuka maneno ya Prof. Bagandanshwa kuwa katika utetezi wa haki za watu wenye ulemavu tunaambatanisha maana katika kila tukifanyacho katika utetezi huo (in every action we do for advocating people with disabilities there must be meaningful context attached to it).
Nakumbuka pia maneno ya rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa akihutubia jumuia wa wana SEKOMU tarehe 9 July, 2014 alisema: "Sasa tunajua, tunapotakiwa kujua habari za elimu maalum tunawauliza watu wa SEKOMU".
Ninaamini kuwa SEKOMU, mbali na taaluma zingine zinazotolewa hapo, kitaendelea kukumbukwa hasa kwa ajili ya elimu maalum.
Sherehe ya kuwapandisha vyeo ngazi ya uprofesa.
Waliopandishwa vyeo ni Dr. Edward Bagandanshwa
(wa kwanza kutoka kushoto, na Dr. Mbatia (wa tatu kutoka kushoto)
|
Stafu ya SEKOMU wakati wa hafla ya kuwapandisha
vyeo kitaaluma Dr. Bagandanshwa na Dr. Mbatia kuwa profesa.
|
Ustaarabu huu mzuri wa Elimu Maalum kwa vyuo vikuu umeanzia SEKOMU, tunahitaji sasa kuueneza kwenye vyuo vikuu vingine nchini. Hii ni kwasababu, watu wenye mahitaji maalum ni wengi, wapo mijini na vijijini, wakubwa kwa wadogo. Tunahitaji kujenga jamii jumuishi ambayo kila mtu anathubutu kumjumuisha mwenzake.
Viva SEKOMU...
No comments:
Post a Comment